Nafasi Ya Matangazo

February 23, 2010


BENDI kongwe ya muziki wa Dansi nchini ya Msondo Music imewanyakuwa waimbaji, Hamisi Tenguweni'Super Maliki' akitokea bendi ya Makoba ambapo amewai kuimbia bendi ya TOT plas na Shikamoo Jazz zote za jijini Dar es salaam pamoja na Mohamedi Mwerevu 'Muddy Clever' akitokea bendi ya Maruni Komando,ambapo ameshawai kuimba katika bendi za Nyota Sound Afrika na Lessi Wanyika zote za Kenya

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa kundi hilo, Rajabu Mhamila 'Super D'
Alisema, wameamua kuwachukuwa waimbaji hawo kwa kuwa wana uwezo wa kuisaidia bendi na sasa wameshaanza kupanda katika jukwaa la bendi hiyo ambapo mpaka sasa tunajipanga kutoa nyimbo mpya za mwaka uhu baada ya mwaka jana kutambulisha albamu yetu ya huna shukrani na kuwa ipo mtaani kwa sasa inauzwa,

Wakati huohuo, bendi hiyo kwa sasa imekuwa ikitoa burudani za wazi katika kuwaweka karibu wapenzi wake ambapo kila jumamosi tunakuwa katika viwanja vya TCC Chan'gombe na jumapili huwa tupo jijini Dar es Salaam na mpaka sasa tuna nyimbo mbili mpya moja ni Lipi jema uliotungwa na Eddo Sanga na Dawa ya Deni kulipa wa Isihaka Katima 'DJ Papa upanga'

Alisema, sambamba na burudani hizo pia wamejipanga kutoa nyimbo mpya kila baada ya wiki tatu ili kukamilisha albamu ya mwaka uhu mapema kadri iwezekanavyo alisema Mhamila,
Akitoa wito kwa wapenzi wa bendi hiyo kuhudhulia kuona maonesho yao popote yafanyikapo kwani kuna burudani ambazo azihitaji kuadithiwa

Mwisho.
Posted by MROKI On Tuesday, February 23, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo