Mpigania Uhuru na Waziri Mkuu Msataafu wa Serikali ya Kwanza ya Tanzania, Mzee Rashid Mfaume Kawawa "Simba wa Vita" amefariki dunia leo asubihi alipolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Mzee Kawawa pia ni Muasisi wa Chama cha Mapinduzi na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Pia atakumbukwa kwa kupenda michezo hasa mchezo wa bao ambapo katika uhai wake alikuwa ni Mlezi wa chama cha Michezo ya jadi CHAMIJADA mkoa wa Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Rashid Mfaume Kawawa aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jana jioni kabla ya kufikwa na Umauti leo saa 9:25 asubuhi.
Rais Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akifurahi jambo na Mzee Kawawa na Daktari wake jana.
Rais Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akifurahi jambo na Mzee Kawawa na Daktari wake jana.






0 comments:
Post a Comment