Mfungwa atunukiwa Shahada ya Sheria Ukonga
Kwamara nyingine tena Mfungwa katika gereza la Ukonga Dar es Salaam ametunukiwa Shahada ya Sheria ya chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT). Ernest Michael (30) pichani alitunukiwa Shahada hiyo leo katika viwavya vya KM Garden Magereza Ukonga na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Dk. Samuel Malecela katika mahafali ya aina yake na yapekee. Michael anatumikia kifungo cha miaka kumi jela kwa kosa la kukuta na madawa ya kulevya akiwa nchini Maritus na alianza kifungo chake nchini humo tangu mwaka 2001 kabla ya kuhamishiwa Ukonga miaka minne iliyopita na kujiunga na chuo hicho kwa masomo. Mfungwa wa kwabnza kutunikiwa Shada ya sheria akiwa gerezani ni Haruna Gomela ambaye sasa anasoma Mastars ya sheria.
December 01, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)






0 comments:
Post a Comment