Nafasi Ya Matangazo

November 11, 2009

Mzee Ojjiki wa Sunderland na Mary Black Bird afariki duniaMchezaji wa zamani wa Timu ya Sunderland hivi sasa Simba, Joseph Laurence Ojjiki (77) a.k.a Msalaba, (pichani) amefariki dunia juzi jijini Dar es salaam na kuzikwa Novemba 11, 2009 katika makaburi ya Kinondoni jijini.

Ojjiki aliyezaliwa Juni 02, 1932 alifariki Novemba 08, 2009 baada ya kuugua ghafla.

Mbali na kuichezea timu ya Sunderland pia alikuwa akiichezea timu ya Taifa ya Tanganyika katika michuano ya Gossage siku hizi Challenge Cup katika mika ya 1950's.

Mbali na kulisakata gozi la Ng'ombe pia Ojjiki ni mmoja wa waanzilishi wa kundi la muziki la Mary Black Birds akiwa na Mzee Ally Sykes.

Marehemu Ojjiki ameacha watoto 3 wajukuu 12 na vitukuu 8.
Blogu hii ya jamii inawapa pole wanafamilia wote, ndugu jamaa na marafiki waliokubwa na Msiba huo mzito.
Kipekee tunaipa pole familia ya Jaji. Joseph Sinde Warioba, Familia ya Michael Maluwe na Familia ya Mwombela-Marekani.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Mungu lihimidiwe Amina.
Posted by MROKI On Wednesday, November 11, 2009 1 comment

1 comment:

  1. Familia ya Ojiki, tumepokea kwa majonzi kifo cha Baba. Mungu amlaze Baba Mzee Ojiki mahali pema peponi.

    Kutoka Familia ya Mwombela, USA

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo