Nafasi Ya Matangazo

September 21, 2024







Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa Tanzania (SHIMIWI) pamoja na baadhi ya klabu zake zinazoshiriki kwenye michezo ya mwaka 2024 mkoani Morogoro, wamepata udhamini wa vifaa na jezi kutoka Benki ya NMB.

Akikabidhi vifaa ambavyo ni mipira ya michezo ya soka na netiboli pamoja na jezi na suti za michezo (trucksuit), Meneja Mwandamizi wa Huduma za Kibenki kwa upande wa Serikali, Amanda Feruzi amesema wametoa vifaa hivyo baada ya kupokea maombi kutoka kwa wahusika.

Amanda amesema kwa upande wa SHIMIWI huu ni mwaka wa tatu tangu waanze kuwadhamini kwa kuwapatia suti za michezo, wakati kwa upande wa klabu za michezo ambazo amezitaja kuwa ni Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Utratibu, Wizara ya Ardhi,  Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Elimu na Wizara ya Katiba na Sheria, baadhi zimekuwa zikifadhiliwa.

“Tunashukuru kwa kuendelea kutuamini kama benki na kushirikiana na sisi mkiwa ni watumishi wa umma, mbali na kufanya biashara pia tumekuwa na ushirikiano katika michezo na leo tumeshughudia klabu tulizozidhamini kuongezeka kutoka tatu na sasa zimekuwa sita,” amesema Amanda.
  
Hatahivyo, amesema kuwa wamekuwa wadau wakubwa wa michezo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anayehimiza watanzania kushiriki kwenye michezo ili kulinda afya.  

Ufadhili huo kwa ujumla umegharimu kiasis cha shilingi milioni 24.5 za Kitanzania, ambapo wameahidi kuendelea kutoa ufadhili pindi watakapoombwa kufanya hivyo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa SHIMIWI, Alex Temba amewashukuru NMB kwa kuwa karibu na shirikisho hilo, na amewataka kutoa elimu za akaunti mbalimbali zilizopo kwenye benki hiyo kwa watumishi wanaoshiriki michezo hii kwenye viwanja mbalimbali.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Michael Masubo amewakaribisha wananchi wa mkoa wa Morogoro na vitongoji vyake kutembelea kwenye viwanja vya Jamhuri, Chuo cha Ujenzi, Shule ya Sekondari ya Morogoro, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kampasi kuu na kampasi ya Mazimbu, ili kujipatia burudani zinazotolewa na watumishi wa umma.

Masubo ameitaja michezo inayochezwa kuwa ni mpira wa miguu, netiboli, kuvuta kamba, riadha, mbio za baiskeli, draft, karata, bao na darts.
MWISHO
Posted by MROKI On Saturday, September 21, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo