Nafasi Ya Matangazo

November 11, 2009

Mamba yakubwa na mafuro 20 wapoteza maishaMafuriko makubwa yamekikumba kijiji cha Manka kilichopo Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro na watu 20 wanaripotiwa kupoteza maisha na maelfu kupoteza makazi.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema watu waliotambulika hadi jana ni wanafunzi saba wa shule ya msingi Miamba Mamba.

Maiti waliotambuliwa ni Elitabu Shambi, Napenda Bakari, Nashemba bakari, Nati John, Mariamu Juma, Ndimangwa Elineema, Amani Mhina, Ruth Mhina, Kiondo Amani, Neema Bakari. Maiti wengine hadi jana jioni bado walikuwa hawajambuliwa.

Kijiji hicho kina watu zaidi ya 1500.
Mafuriko hayo yametokea kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo na mikoa mingine nchini. Taarifa zaidi tutaendelea kuwapa.
NB: Picha hiyo haihusiani na Mamba.
Posted by MROKI On Wednesday, November 11, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo