Nafasi Ya Matangazo

November 10, 2009

Mamlaka ya mapato nchini TRA kupitia wakala wake wa ukusanyaji madeni sugu kampuni ya MAJEMBE AUCTION MART "Vijana wa Kazi" leo wamepiga kufuli mali za kampuni ya kufua umeme ya DOWANS kutokana na TRA kuidai kampuni hiyo shilingi za kitanzania Bilioni 9,120,611,746 ya kodi zake mbalimbali.
Pichani juu ni baadhi ya mali za kampuni hiyo ya Dowans ambazo leo zimepigwa kufuli na iwapo deni hilo hatolipwa ndani ya siku 10 kuanzia leo mali hizo na mitambo itapigwa mnada hadharani.
Minyororo katika geti la dowans
Emmanuel Wambando wa kampuni ya Udalalai ya Majembe akionesha kufuli.
baadhi ya mitambo iliyopo ndani...
Mkurugenzi wa Majembe, Seth Moto akionesha moja ya magari yaliyokamtwa .
Posted by MROKI On Tuesday, November 10, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo