
Mkazi wa Kijiji cha Ntatumbila wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Christant Nkoswe akizungumza mbele ya timu ya watalaamu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, waliotembelea kijiji hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, Mhandisi Emmanuel Kalobelo akizungumza na wananchi kwenye Kijiji cha Songambele wilayani humo wakati wa kuhamasisha matumizi ya vocha za ruzuku za pembejeo za kilimo na mpango wa Kilimo Kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita. Kulia ni Mchumi kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Hashim Kimomwe.

Wakazi wa Nkasi, Danny Kelvin (kulia) na Dismas Norman wakijaza mahindi kwenye gunia tayari kuyapima kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kilichoko Nkasi mkoani Rukwa juzi. Kituo hicho kina uwezo wa kuchukua tani 300 za mahindi.

Magunia ya mahindi yakiwa yamelundikana nje ya Kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), wilayani Nkasi mkoani Rukwa juzi. Kituo hicho kwa sasa kinakusanya mahindi na kina uwezo wa kuchukua tani 300 za mahindi.
0 comments:
Post a Comment