
Wanafunzi wa shule ya Msingi Kilimani iliyopo kitunda wilaya ya Ilala wakiwa wamekaa chini darasani na mwalimu wao akiwafundisha hii ni kutokana na uhaba wa madawati mashuleni.Vodacom Foundation imewapatia msaada wa madawati 70 ikiwa ni kampeni yake ya kutoa msaada wa madawati 400 katika shule za msingi mkoa wa Dar es Salaam wenye thamani ya zaidi ya milioni 32.

Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba(kulia)akimkabidhi Diwani wa kata ya kitunda Osango Kaseno moja ya madawati kati ya 70. Katikati ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Josephine Matiku.
0 comments:
Post a Comment