
Wapenzi wa timu ya Simba Joel Bendera (kushoto) Prof . Juma Kapuya (katikati) na Samuel Sitta wakijadili jambo katika siku ya tamasha la michezo la Simba.

Mgeni rasmi Samuel Sitta akizindua 'uzi' zitakazo tumika katika ligi msimu huu na wekundu wa Msimbazi.

Vijana wakipasha moto misuli tayari kwa ligi kuu 2009/2010.

Kikosi cha Simba kilicho ichapa goli 1-0 Villa ya Uganda katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam katika tamasha la Simba.

Villa ya Uganda waliokubali kichapo cha goli 1-0 toka Simba.

Mgeni rasmi Samuel Sitta akihojiwa na Abdala Majura wa BBC.

Burudani ya ngoma ikitumbuiza mamia ya mashabiki na wapenzi wa Simba waliojitokeza katika tamasha la Simba uwanja wa Uhuru Dar es Salaam leo. Blogu hii ya jamii inawatakia kila la heri Simba 2009/2010.
0 comments:
Post a Comment