Naibu Katibu Mkuu (Mazingira)
Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda akikabidhiwa mitambo mitambo mitatu
ya utambuzi wa kemikali zinazotumika kwenye viyoyozi na majokofu kutoka kwa
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO)
Bi. Lorence Ansermet katika hafla iliyofanyika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais
jijini Dar es Salaam Mei 28, 2026.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira)
Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda akikabidhi mitambo mitambo mitatu
ya utambuzi wa kemikali zinazotumika kwenye viyoyozi na majokofu kwa Mkufunzi
kutoka Chuo cha Mafunzo ya Amali cha Mkokotoni Zanzibar Bw. Haji Khamis Haji
iliyotolewa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO) Bi. Lorence
Ansermet katika hafla iliyofanyika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais jijini Dar es
Salaam Mei 28, 2026.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira)
Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO) Bi. Lorence
Ansermet wakimsikiliza Mkufunzi kutoka Wakala wa Mafunzo ya Elimu ya Uvuvi
Bagamoyo (FETA) Mhandisi Goodluck Lulagora wakati akitoa maelezo kuhusu
namba mitambo utambuzi wa kemikali zinazotumika kwenye viyoyozi na majokofu inavyofanya
kazi wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais
jijini Dar es Salaam Mei 28, 2026.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira)
Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda (kulia) akzungumza na Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO) Bi. Lorence
Ansermet katika hafla ya makabidhiano ya mitambo mitambo mitatu ya utambuzi wa
kemikali zinazotumika kwenye viyoyozi na majokofu iliyofanyika Ofisi ndogo ya
Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam Mei 28, 2026.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira)
Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda (wa tatu kushoto) na Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO) Bi. Lorence
Ansermet kwakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa
Rais na wakufunzi kutoka vyuo wakufaika wa mitambo mitambo mitatu ya utambuzi
wa kemikali zinazotumika kwenye viyoyozi na majokofu baada ya hafla ya
mabadhiano iliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais jijini Dar es
Salaam Mei 28, 2026.
*****************
Naibu
Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda amepokea mitambo
mitatu ya utambuzi wa kemikali zinazotumika kwenye viyoyozi na majokofu pamoja
na mitambo ya kusafisha kusafisha kemikali hizo na kuzichakata kwa ajili ya matumizi
bila kutegemea kuagiza nje nchi.
Mitambo
hiyo imetolewa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO)
kupitia kwa Mwakilishi Mkazi wa Bi. Lorence Ansermet katika Ofisi ndogo
ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam leo Mei 28, 2026.
Hatua hiyo ni mojawapo ya jitihada za Serikali za kulinda
mazingira ambapo mitambo hiyo itatumika katika uvunaji, uchakataji na kutumia
tena badala ya kuziachia kwenda kuharibu tabaka la ozoni.
Mitambo hiyo itakabidhiwa
katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia
Mbeya (MUST), Chuo cha Mafunzo ya Amali cha Mkokotoni, Zanzibar pamoja na
Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Bagayamo, Pwani.
Akizungumza mara baada ya
kupokea mitambo hiyo, Balozi Luvanda alisema tukio hilo linaonesha dhamira endelevu ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na washirika wake katika kuimarisha elimu ya
ufundi, ufundi, utunzaji wa mazingira na maendeleo endelevu ya viwanda.
Alisema vifaa vilivyokabidhiwa si
mashine tu bali ni uwekezaji katika maarifa, ukuzaji ujuzi, uvumbuzi, na
mustakabali wa mafundi na wataalamu wetu wachanga, hivyo alitoa wito kwa
wanufaika wavitunze ili vidumu kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Mwakilishi
Mkazi wa UNIDO Bi. Lorence alisema hatua hiyo ni matokeo ya Tanzania kujiunga
na Mkataba wa Vienna
wa Ulinzi wa Tabaka la Ozoni na Itifaki ya Montreal kuhusu vitu vinavyopunguza Tabaka
la Ozoni tangu mwaka 1993.
Alisema mitambo hiyo itasaidia
katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo husababisha joto kali
katika uso wa duniani kutokana na kuharibiwa kwa tabaka la ozoni.
Bi. Lorence aliongeza UNIDO na Ofisi
ya Makamu wa Rais zitaendelea kushirikiana ili kuongeza ufanisi katika
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuendelea kutoa mafunzo kwa mafundi
mchundo wa majokofu na viyoyozi.
Akitoa maelezo ya awali
Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Thomas Chali
alisema Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotekeleza mpango wa kudhibiti kemikali
zinazoharibifu tabaka la ozoni aina ya hydrochlorofluorocarbons ifikapo mwaka
2030.
Bw. Chali alisema kuwa UNIDO imekuwa na mchango mkubwa
katika utekelezaji wa mpango wa kuondosha kemikali hizo utoaji wa vifaa vya kuudumia
majokofu na viyoyozi pamoja na programu za kujenga uwezo na mafunzo ya
kiufundi.
Alisema Tanzania imekuwa Mshirika wa Mkataba wa Vienna wa
Kulinda Tabaka la Ozoni na Itifaki ya Montreal juu ya Vitu Vinavyoharibu Tabaka
la Ozoni tangu Aprili 1993.
Vifaa vya Kupunguza Uharibifu wa Ozoni (ODS) vinatumika
katika sekta mbalimbali, hasa katika huduma za majokofu na viyoyozi. Ofisi ya
Makamu wa Rais ni kiungo cha kitaifa na mamlaka yenye uwezo wa utekelezaji wa
mikataba hii ya kimataifa nchini.
0 comments:
Post a Comment