Nafasi Ya Matangazo

March 27, 2009

RAIS Jakaya Kikwete (pichani) kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani 2005 mepangua safu ya ma DC (wakuu wa wilaya) kwa kuteua wapya 15, kustaafisha saba na kuwabadilisha vituo 54.

Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), imebainisha ma DC wawili watapangiwa kazi nyingine na wengine wawili wameondolewa baada ya hivi karibuni kuteuliwa kuongoza Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mabadiliko haya yanatarajiwa kuongeza chachu katika usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake.

Wakuu wapya na wilaya zao kwenye mabano ni Mercy Silla (Arumeru), Norman Sigalla (Hai), Kanali Issa Njiku (Misenyi), Angelina Mabula (Karagwe), Dk. Rehema Nchimbi (Newala), Francis Isaac (Mbulu), Luteni Kanali Benedict Kitenga (Rorya) na Luteni Kanali Cosmas Kayombo (Mbarali).

Wengine ni Christopher Kangoye (Kwimba), Queen Mlozi (Ukerewe), Fatuma Mwassa (Mvomero), Fatma Ally (Nanyumbu), Juma Madaha (Tunduru), Anatory Choya (Kishapu) na Erasto Sima (Korogwe).

Waliostaafishwa ni Elias Maarugu (Misenyi), Deusdedit Mtambalike (Muleba), David Holela (Babati), Hawa Ngulume (Mbarali), Mashimba Mashimba (Kyela), Kanali Peter Madaha (Nyamagana) na Gilbert Dololo (Kibaha).

Wanaosubiri kupangiwa kazi nyingine ni Patrick Tsere (Ilala) na Doreen Kisamo (Uyui).

Martin Shigela aliyekuwa Lindi aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM wakati Husna Mwilima aliyekuwa Hai, aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT).

Wakuu wa wilaya waliobadilishwa vituo vya kazi ni wafuatao: Elias Lali (kutoka Arumeru kwenda Ngorongoro), Evans Balama (Arusha kwenda Ilala), Jowiko Kasunga (Ngorongoro kwenda Monduli), Kanali Fabian Massawe (Kinondoni kwenda Muleba), Abdallah Kihato (Temeke kwenda Kyela) na Zainab Kwikwega (Bahi kwenda Kasulu).

Wengine ni Dk. Ian Langiboli (Chamwino kwenda Babati), Kapteni Seif Mpembenwe (Kondoa kwenda Handeni), Halima Dendego (Mpwapwa kwenda Kilosa), Lephy Gembe (Makete kwenda Chamwino), Elaston Mbwilo (Iringa kwenda Mtwara) na Darry Rwegasira (Njombe kwenda Mpwapwa).

Waliohamishwa wengine ni Said Mkumbo (Chato kwenda Temeke), Frank Uhahula (Karagwe kwenda Tarime), Luteni Kanali John Mzurikwao (Kibondo kwenda Mpanda), Saidi Bwanamdogo (Kasulu kwenda Kondoa), Raymond Mushi (Rombo kwenda Arusha) na Jordan Rugimbana (Mwanga kwenda Kinondoni).

Wakuu wa wilaya wengine waliohamishwa vituo ni Rashid Ndaile (Nachingwea kwenda Chunya), Anna Magowa (Liwale kwenda Hanang), Elias Goroi (Mbulu kwenda Nachingwea), Kapteni Geoffrey Ngatuni (Hanang kwenda Musoma), Saveli Maketta (Musoma kwenda Namtumbo) na Stanley Kolimba (Tarime kwenda Uyui).

Wengine ni Miriam Lugaila (Rungwe kwenda Misungwi), Halima Kihemba (Mbozi kwenda Kibaha), Fatuma Kimario (Chunya kwenda Igunga), Athuman Mdoe (Kilosa kwenda Mwanga), Hawa Ng’humbi (Mvomero kwenda Makete),
Gishuli Charles (Mtwara kwenda Njombe) na Jackson Msome (Newala kwenda Rungwe).

Wengine waliohamishwa ni Kapteni Assary Msangi(Nanyumbu kwenda Iringa), Samwel Kamote (Ilemela kwenda Bukoba), Danhi Makanga (Kwimba kwenda Kibondo), Magalula Magalula (Misungwi kwenda Lindi), Paul Chiwile (Ukerewe kwenda Liwale) na Mathew Nasei (Magu kwenda Muheza).

Wakuu wengine waliohamishwa ni Luteni Kanali Serenge Mrengo (Bagamoyo kwenda Ilemela), Ali Rufunga (Rufiji kwenda Manyoni), Meja Bahati Matala (Sumbawanga kwenda Kahama), Thobias Mazanzala (Mpanda kwenda Sumbawanga) na Gabriel Kimolo (Namtumbo kwenda Mbozi).

Pia wengine ni Peter Kiroya (Tunduru kwenda Rombo), Amina Masenza (Mbinga kwenda Shinyanga), Khadija Nyembo (Kishapu kwenda Chato),
Kanali mstaafu Edmund Mjengwa (Shinyanga kwenda Mbinga) na Magesa Mulongo (Bukombe kwenda Bagamoyo).

Wengine ni Florence Horombe (Singida kwenda Bukombe), Pascal Mabiti (Manyoni kwenda Singida), Cleophas Rugarabamu (Igunga kwenda Nyamagana), Kassim Majaliwa (Urambo kwenda Rufiji), Luteni Winfrid Ligubi (Handeni kwenda Urambo), Elizabeth Mkwasa (Korogwe kwenda Bahi) na Zainab Kondo (Muheza kwenda Magu).
Posted by MROKI On Friday, March 27, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo