Nafasi Ya Matangazo

October 03, 2016

Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akiongea na Waandishi wa vyombo vya habari juu umuhimu wa uwekaji wa akiba duniani. Kulia ni Meneja Masoko wa TPB, Grace Majige na Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki, Timotheo Mwakifulefule.
Mteja wa TPB tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akiongea na Waandishi wa vyombo vya habari juu ya faida alizozipata kutoka na kuweka akiba katika benki hiyo. Kushoto kwake niMeneja wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya na Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki, Timotheo Mwakifulefule (kulia)
Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akimpa zawadi ya benki moja ya wateja wa tawi hilo Alex Lwamanya katika uzinduzi wa mwezi wa akiba duniani. Kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki, Timotheo Mwakifulefule

Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akimpa zawadi ya benki moja ya wateja wa tawi hilo Grace Mgala katika uzinduzi wa mwezi wa akiba duniani. Kushoto ni Afisa Mwandamizi wa huduma kwa wateja, Glory Mutta.
Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akimpa zawadi ya benki moja ya wateja wa tawi hilo Mohammed Salim katika uzinduzi wa mwezi wa akiba duniani.


Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akimpa zawadi ya benki moja ya wateja wa tawi hilo Jumanne Waziri katika uzinduzi wa mwezi wa akiba duniani. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI


BENKI ya Posta nchini (TPB) imezindua mwezi wa uwekaji akiba duniani inayokwenda sambamba na kampeni iliyopewa jina la “Asante Mteja”.


Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi huo, Meneja wa benki ya TPB tawi la Kariakoo, Patrick Swenya alisema kuwa kampeni hiyo itaendeshwa nchi nzima katika matawi yao. Alisema, lengo la kampeni hiyo ni kuhamasisha wateja wa TPB kuweka akiba ili kuweza kufanikisha malengo yao katika maisha ikiwemo ulipaji wa ada za wanafunzi. 

Meneja huyo alisema kuwa katika kuhakikisha wateja wao wanafanikiwa watatoka na kutembelea wateja wao ambao wengi ni wafanyabiashara ili kupata mrejesho wa huduma wanazozitoa ikiwemo mikopo kama imeweza kuwakomboa.

Alisema, kama watabaini mikopo inayotolewa imewanufaisha watu wengi basi watahakikisha inaboreshwa zaidi ili kuwakwamua watu wengi kiuchumi. "Katika wiki hii ya uwekaji akiba duniani tutahakikisha sisi kama TPB tunaboresha huduma zetu ili kufanikisha zaidi Watanzania ikiwa pia ni moja ya njia ya kuwashukuru kwa kuchagua Benki yetu", alisema Swenya. Aidha aliongeza kuwa TPB itaendelea kuboresha huduma ikiwemo mikopo ya vikundi visivyo rasmi inayotolewa kwa riba nafuu.

Kwa upande wake mmoja wa wateja wa benki hiyo Alex Lwamanya alisema kuwa mikopo ya riba nafuu inayotolewa na benki hiyo imeweza kumkwamua kiuchumi kwa kiasi kikubwa.

Alisema, hadi sasa mikopo hiyo imemuwezesha kujenga nyumba pamoja na kuendeleza biashara zake. "Nashkuru mikopo niliyoipata na ninayoendelea kupata imenikwamua kimaisha kwa kiasi kikubwa sana kwani hadi sasa nimeweza kumiliki vitega uchumi vinavyoniingizia kipato", alisema Alex.
Posted by MROKI On Monday, October 03, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo