Nafasi Ya Matangazo

November 11, 2015

MISS Tanzania 2014, Lilian Kamazima anataraji kuwakilisha Tanzania katika shindano la Miss World lilipangwa kufanyika Desemba 19 mwaka huu katika ukumbi wa Beauty Crown Grand Theatre ulipo mji wa Sanya, China.

Shindano hilo la urembo duniani lenye hadhi ya kimataifa litashirikisha warembo kutoka mataifa 120 toka duniani kote.

Mrembo huyo wa Tanzania  pamoja na warembo wengine watakaa katka Hotel ya Beauty Crown Sanyakatika kambi yao itakayoanza Novemba 21 mwaka huu hadi siku ya fainali hizo.

Afisa habari wa kampuni ya Lino International Agency ambao ndio waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hidan Rico, amesema Miss Tanzania anataraji kuondoka nchini Novemba 19, kuelekea katika kambi ya mashindano hayo.

Rico amesema maandalizi ypote muhimu kwaajili ya safari ya mrembo huyo yamekamilika na mrenbo anaendelea kujifua.

"Maandalizi kwaajili ya safari ya mrembo wetu, yamekamilika na kwa sasa anaendea na mazoezi ya kujiweka sawa,"alisema Rico.

Kisiwa cha Sanya China kimekuwa wenyeji wa mashindano ya urembo ya dunia kwa muda wa miaka mingi tangu mwaka 2005 na mwaka huu pia washiriki wanatarajia kufurahi na kujiona utajiri na utalii wa China.

Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo iliyotolewa na waandaaji wa shindano hilo, washiriki wote watapata fursa ya kutembela sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na sehemu maalum ya ukuta wa China sehemu ambayo imekuwa  kivutio kikubwa kwa watalii wanaotembelea China.

Washiriki wote wamehamasishwa kutumia Mitandao ya Jamii kwa madhumuni ya kujitangaza wenyewe na pia kutangaza utalii wa China pamoja na shindano kubwa lenye hadhi ya kimataifa Shindano la urembo la Dunia.

Mitandao hiyo ya Jamii pia itatoa Alama (Marks) kwa washiriki wote watakaofanya vizuri katika kutumia Mitandao hiyo, Alama ambazo pia zitasaidia katika kuongeza nafasi za ushindi katika shindano hilo.

Afisa habari wa kampuni ya Lino International Agency ambao ndio waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hidan Rico amesema hii ni fursa pekee kwa watanzania kumpa ushindi mrembo wao.

“Tunawaomba Watanzania kutembelea Mitandao hiyo ya  mrembo wetu wa Tanzania, facebook pamoja na twitter ili kumpa sapoti na kumuongezea Alama mrembo wetu,”alisema Rico.

Tunawaomba pia Watanzania wote wanaoishi hapa nchini pamoja na wale wa Nchi za nje wenye uwezo kuhudhuria Fainali za Shindano la urembo la Dunia litakalofanyika tarehe 19 Desemba 2015 katika ukumbi wa Beauty Crown Grand Theatre uliopo Sanya china.
Posted by MROKI On Wednesday, November 11, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo