KIKOSI cha wachezaji 24 wakiwepo nyota wanaokipiga nje ya mnchi wa timu ya Taifa ya Algeria kinatarajiwa kuwasili Tanzania kesho kwa ndege binafsi ya kukodi.
Msafara
huo utakuwa na watu 65 ambapo kati yao wachezaji 24 watawasili tayari kwa mchezo wa Jumamosi Novemba 14
dhidi ya wenyeji Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha
mkuu wa timu hiyo Christian Gourcuff raia wa Ufaransa ametaja kikosi
cha wachezaji 24, wakiwemo wachezaji 18 wanaocheza katika klabu za Ulaya
kwa ajili ya kuikabili Tanzania.
Mchezo huu wa raundi ya pili ni
wa kuwania kuingia katika hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kombe la
dunia litakalofanyika huko nchi Urusi mwaka 2018.
Kikosi hicho cha Algeria, kitaongozwa na kiungo
mshambuliaji, anaekipiga na timu ya Tottenham, Nabil Bentaleb.
Wegine katika orodha hiyo ya wachezaji 18
wanaocheza soka la kimataifa nje ya Algeria na timu zao katika mabano ni pamoja
na Brahimi Yassine (Porto), Sofiane Feghouli (Valencia), Slimani Islam
(Sporting Lisbon), Abeid Mehdi (Panathinaicos), Ryad Boudebouz (Montpellier),
Saphir Taider (Bologna) na Zeffane Mehdi (Rennes).
Wengine ni pamoja na Benrhama Said (Nice), Soudani
Hilal Al Arabi (Dinamo Zagreb), Mesbah Djamel Eddine (Sampdoria), Rachid Ghezzal
(Lyon) na Walid Mesloub (Lorient).
Wakali hao wataumana na Taifa Star iliyo na
wachezaji wengi, wanaocheza soka la ndani ukiacha nyota wa ufungaji magoli
Afrika, Mbwana Samatta anaekipiga na Mabingwa wa soka Afrika, TP Mazembe na
mwenzake Thomas ulimwengu. Wengine ni Mrisho Ngasa.
0 comments:
Post a Comment