Nafasi Ya Matangazo

October 07, 2015

Mkutano wa Mkuu wa Pili wa Chama cha Kudhibiti Mbu cha Pan African (PAMCA) leo umeingia katika siku yake ya pili jijini Dar es Salaam ambapo watafiti wamewasilisha taarifa zao mbalimbali za utafiti walizofanya katika maeneo yao kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwa ni pamoja na ushauri wa kitaalam wa kupata suluhisho la kumdhibiti na hatimaye kumtokomweza kabisa Mdudu mbu barani Afrika. Pichani ni Mwanasayansi Mtafiti Kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dk Bilali Kabula akiwasilisha taarifa yake. Mkutano huo wa siku tatu ulianza Oktoba 6 na utamalizika Oktoba 8, 2015.
 Dk Kabula kutoka NIMR aliwasilisha taaifa ya utafiti uliofanywa jijini Dar es salaam kuangalia vinasaba vinavyosababisha usugu wa mbu waenezao Malaria dhidi ya viuatilifu.

Matokeo ya utafiti huo yalionesha kuwepo kwa vinasaba vinavyosababisha mbu wa Malaria kumeng'enya viuatilifu na kufanya kuwa sugu.

Aidha Dk Kabula alisema kuwa na vinasaba vya "KDR" (Knockdown Resistance)vinavyosababisha usugu zaidi ya viuatilifu. 

Ili kudhibiti uenezaji wa vinasaba hivyo, ameshauri matumizi ya viuatilifu aina ya organophosphates na carbonates badala ya pyrethroid. 

"Dawa nyingi hasa zilizopo nchini ambazo watu huzitumia kupulizia mbu majumbani haziwaui na badala yake mbu hao kuzirai tu kwa muda flani na baade kuzinduka na kuendelea tena na kuuma na kueneza maambukizi ya malaria, hivyo dawa mbadala hazina budi kuanza kutumika kupulizia mbu majumbani," alisema Dk Kabula. 

 Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa leo katika mkutano huo katika siku yake ya pili.
 Mmoja wa wanasayansi watafiti akichangia mad. PICHA ZAIDI BOFA HAPA
 Washiriki wakifuatilia kwa makini mada na maoni mbalimbali juu ya namna ya kumdhibiti mdudu mbu barani Afrika.
 Watoa mada wakisubiri maoni ya washiriki
 Mada zilitolewa mkutanoni hapo.


Prof Wencelaus Kilama (kushoto) akishauriana jambo na Watafiti wanasayansi wa Mbu, Dk Bilali Kabula na mwenzake Dk Theresia Nkya wakimsikiliza kwa makini mkongwe huyo wa tafiti za Kisayansi nchini ambaye alipata kuwa Mkurugenzi wa NIMR.

 Katika mkutano huo wa pili wa PAMCA pia kuna maonesho kutoka kwa wadau mbalimbali. Hapa ni katika banda la Taasisi ya Utafiti wa  Kimadawa Kenya (KEMRI), na hapa Mkurugenzi Msaidizi wa KEMRI, Musau Kyanesa (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na timu yake na wageni walio watembelea bandani hapo.
 Prof Wencelaus Kilama akisaini kitabu baada ya kutembelea maonesho hayo.
 Prof Wencelaus Kilama akiangalia moja ya bidhaa zinazo zalishwa na KEMRI.
Washiriki wakiwa katika mabanda yao.
Posted by MROKI On Wednesday, October 07, 2015 1 comment

1 comment:

  1. hongera daktari kwa kazi njema . tuletee dawa zenye long recidual effect zipulizwe kote wanakozaliana mbu

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo