Meneja
Mwandamizi wa Biashara Ndogo na Kubwa wa Benki ya DCB, Haika Machaku
akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kuwapatia shuhulisho la masuala ya kifedha wateja na kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara zao
ameyasema hayo leo katika hafla ya kusherekea wiki ya huduma kwa
wateja iliyofanyika makao makuu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja
Mwandamizi wa Technolojia ya Habari na mawasiliano Mohamed Mtulia
.Meneja Masoko wa Benki ya DCB,Boyd Mwaisame akisisitiza jambo katika hafla
ya kusherekea wiki ya huduma kwa wateja, kulia ni Meneja Mwandamizi
wa Biashara Ndogo na Kubwa wa Benki ya DCB, Haika Machaku.
Meneja
Mwandamizi wa Biashara Ndogo na Kubwa wa Benki ya DCB, Haika Machaku
akikata keki na wateja wa Benki hiyo katika hafla ya kusherekea wiki ya
huduma kwa wateja iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo leo jijini Dar
es Salaam.
************
WAJASIRIAMALI nchini wametakiwa kuacha kuhofia kuchukua mikopo katika benki mbalimbali kwa kuogopa kutozwa riba kubwa.
Hatua
inakuja kutokana na kuonekana bado kuna idadi kubwa ya wajasiriamali
wanaobuni bidhaa mbalimbali lakini wanakwama kutokana na kutokuwa na
mtaji wa kutosha wa kuendeleza biashara zao.
Akizungumza
jijini hapa leo na waandishi wa habari, meneja mwandamizi wa biashara
ndogo na kubwa, kwa niaba ya mkurugenzi msaidizi wa Benki ya biashara ya
Dar es salaam (DCB), Haika Machaku, amesema kuwa wajasiriliamali
wanatakiwa kujijengea desturi ya kuchukua mikopo ili kujiendeleza katika
shughuli za kimaendeleo.
“Tunaahidi
kuwapatia shuhulisho la masuala ya kifedha ambao situ katika kuongeza
kasi ya ukuaji wa biashara zenu lakini pia kuwahamasisha ninyi
kufanikiwa zaidi hivyo katika wiki hii ambayo ni ya huduma kwa wateja
tunakataka wajasiriamali ”amesema Machaku.
Aidha
amesema kuwa katika wiki hiyo wanatarajia kutoa huduma mbalimbali
sambamba na kusikiliza maoni ya wateja kuhusiana na huduma zinazotolewa
na benki hiyo.
“Lengo
letu siku zote ni kutoa huduma bora kewa haraka na zenye kukidhi
matakwa ya wateja lakini katika huduma tutakazozitoa ni pamoja na
kuendeleza huduma ya mikopo ya nyumba na uboreshaji wa nyumba” alisema.
Kwa
mujibu wa Machaku amesema mwaka huu wametenga takribani billion 86 kwa
wateja wote kwaajili ya kuwakopesha ili kuwawezesha kukuza biashara zao
na kuongeza kuwa hadi sasa wameshafungua matawi nane katika sehemu
mbalimbali. Source:Michuzi Media.
0 comments:
Post a Comment