Nafasi Ya Matangazo

September 25, 2015


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na aliyekuwa Mbunge wa Ulanga Mashariki, Celine Kombani (56),amefariki dunia hii leo nchini India .



Kombani alipitishwa na Chama cha Mapinduzi kutetea jimbo lake la Ulanga Mashariki na alipita bila kupingwa katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. 



Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa jimbo la Ulanga. 

**********

Anaandika Father Kidevu  


TUJIKUMBUSHE KUHUSU JIMBO LA ULANGA MASHARIKI

JIMBO la Ulanga kabla ya kugawanywa na kutoa majimbo mawili ya Ulanga Magharibi na Ulanga Mashariki lilipata kuongozwa na Mbunge wa zamani wa Ulanga, Nazar Nyoni aliyepata kuwa Naibu Waziri wa Elimu kati ya mwaka 1975 hadi 1980. 



Jimbo la Ulanga liligawanywa na Ulanga Mashariki aliingia Marehemu Guntram Amani Mkolokoti Itatiro, aliyefariki bado akiwa Mbunge 1999 na nafasi yake kushikwa na  Kapteni Mstaafu Theodos James Kasapira ambaye alifariki ghafla akiwa Bungeni Mjini Dodoma akihudhuria kikao cha Bunge la Bajeti Mkutano wa 16 katika Kikao cha 32 kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe Julai 22, 2004.


kisha kuingia Celine Ompeshi Kombani ambae nae amefariki akiwa madarakani na tayari kutetea nafasi yake katika uchaguzi Mkuu unaotaraji kufanyika Oktoba 25, 2015.



ELIMU YA DARASANI

Mamam Kombani alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Kwiro 1968-1975 na baadae kuchaguliwa kujiunga na Sekondari ya Wasichana Kilakala 1975-1978 na kuendelea na kidato cha tano na sita Sekondari ya Wasichana Tabora 1979-1981.



Mwaka 1982 Celine Kombani alijuunga na Taasisi ya Uongozi na Maendeleo Mzumbe (IDM) na kuchukua Shahada ya kwanza ya uongozi na Utawala (B.A) aliyohitimu mwaka 1985.



Mwaka 1994 Celine Kombani alirejea tena IDM Mzumbe ambacho hivi sasa ni Chuo Kikuu Mzumbe (MU) na kusoma Shahada ya Uzamili ya Uongozi na Utawala aliyohitimu 1995.



Pia amepata kuhudhuria semina, Warsha na Makongamano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ambayo yalizidi kumuimarisha katika utendaji kazi wake. 



UONGOZI

Celine baada ya kuhitimu Shahada ya kwanza ya Uongozi na Maendeleo IDM Mzumbe, aliajiriwa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro alipodumu hadi mwaka 1992 kabla ya mwaka 1994 kuajiriwa kiwanda cha Maturubai Morogoro kama Meneja ambako napo alidumu kwa mwaka mmoja na kupata ajira nyingine 1995 Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro kama  Afisa Tawala Mwandamizi, kazi aliyoifanya hadi 2005.



Celene, aliamua kuingia katika siasa na kuwania ubunge katika Jimbo la Ulanga Mashariki katika Uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 2005, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Marehemu Capt (Mstaafu), Theodos James Kasapira, aliyefariki ghafla akiwa Bungeni Mjini Dodoma akihudhuria kikao cha Bunge la Bajeti Mkutano wa 16 katika Mkutano wa 32 kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe Julai 22, 2004.



Baada ya jkurithi mikoba hiyo ya Capt Kasapira, 2006 alichaguliwa kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) alidumu hadi 2008 baraza la mawaziri lilipovunjwa na Edward Lowassa kujiuzulu na Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Pinda kuingia madarakani alipanda na Kuwa Waziri kamili wa TAMISEMI.



Mwaka 2010 aliteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria kabla ya Kuhamishiwa tena Ofisi ya Rais na kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Utumishi) hadi mauti yanamfika.



SIASA

Kwa upande wa Siasa mwaka 1987-1992 alikuwa ni mwanachama wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) na alikuwa mjumbe wa Kamati Maalum ya Chama hicho Kilosa.



Aidha Kombani aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Morogoro  hii ikiwa ni 2002 hadi 2005.
Posted by MROKI On Friday, September 25, 2015 1 comment

1 comment:

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo