Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Ndugu Allan Kijazi akizungumza jambo,wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Wahariri wa Habari Tanzania,mapema leo asubuhi jijini Mwanza.Ndugu Kijazi alisema kuwa Utalii ni sekta mtambuka na inachochea
ukuaji wa sekta nyingine ikiwa ni pamoja na kilimo, usafirishaji wa anga na
barabara, huduma za fedha, huduma za chakula na malazi kudorora kwa sekta
nyinginezo. "Hivyo kudorora kwa sekta
hii huchangia kwa kiasi kikubwa kudorora kwa sekta nyingine. Aidha, hadi sasa, Utalii unaongoza katika
kuingiza fedha za kigeni ikiwa ya kwanza na kufuatiwa na sekta ya madini na
kilimo.
Kwa na kwa ujumla unachangia asilimia 17.5 ya Pato
la Taifa lakini tathmini inaonyesha sekta hii inaweza ikachangia zaidi ya 30%
ya pato la Taifa. Asilimia zaidi ya 80
ya utalii nchini ni utalii wa kutembelea kwenye Hifadhi za Taifa, na hii
inaonyesha kuwa hifadhi hizi ni muhimu kwa ustawi wa taifa letu. Ni zaidi ya mara tatu ya idadi ya
wanaotembelea Hifadhi hizi'',alisema Ndugu Kijazi.
Alisema kuwa Maeneo yaliyo chini ya Hifadhi za Taifa
yana faida nyingi za kiikolojia (ecosystem services) kama vile kuwa vyanzo vya
maji (mfano; Hifadhi za Kilimanjaro, Arusha na Udzungwa). Maji hayo pia
hutumiwa kwa ajili ya kuzalisha umeme unaotumika kwenye gridi ya Taifa. Hivyo
faida za kusimamia Hifadhi hizi haziishii tu kwa watalii kufurahia bali pia
kuna faida nyingine za kiuchumi ambazo sio rahisi sana kuziainisha katika mfumo
wa kifedha (i.e. other values which are
not easily tagged in financial terms).
Ndugu Kijazi alisema mwaka huu 2015, mtandao maarufu wa
kimataifa unaojulikana kwa jina la “Safari Bookings” uliiteua Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti kuwa “The best park
for African safaris” na hii ni baada ya kushindanishwa na hifadhi nyingine
50 Barani Afrika zikiwemo za Afrika Kusini.Aidha, Hifadhi za Mikumi na Arusha zilitunukiwa “Certificate of Excellence”
na mtandao maarufu duniani ujulikanao kama TripAdvisor.
Katika ufunguzi wa Warsha hiyo,Ndugu Kijazi alisema kuwa, Kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka
huu ni “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. aliongeza kusema kuwa pamoja na
kuelezea shughuli za TANAPA, mada zitakazowasilishwa zitahusu masuala ya Utalii
na Uhifadhi na namna wanahabari wanavyoweza kushirikiana na TANAPA katika kuhimiza
uhifadhi na kuendeleza utalii. "Mada kuu
nne zitawasilishwa na viongozi wa TANAPA na wanazuoni maarufu akiwemo Nd.
Jenerali Ulimwengu na Dkt. Alfred Kikoti. Inatarajiwa kuwa washiriki watapata
fursa ya kuchangia na mwishoni watatushauri namna ya kuboresha utekelezaji wa
majukumu yetu",alisema Kijazi.
PICHA NA MICHUZI JR
PICHA NA MICHUZI JR
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa akifafanua jambo katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari na Wana habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano
wa mwaka huu ni “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. Pamoja na
kuelezea shughuli za TANAPA,aidha imeelezwa katika Warsha hiyo kuwa mada zitakazowasilishwa zitahusu masuala ya Utalii
na Uhifadhi na namna wanahabari wanavyoweza kushirikiana nasi katika kuhimiza
uhifadhi na kuendeleza utalii.
Baadhi ya Wahari wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano
wa mwaka huu ni “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. Pamoja na
kuelezea shughuli za TANAPA.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchni (TANAPA),Pascal Shelutete akifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo mapema leo asubuhi jijini Mwanza
Baadhi ya Wahari wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano
wa mwaka huu ni “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. Pamoja na
kuelezea shughuli za TANAPA.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndugu Allan Kijazi pichani kati na Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchni (TANAPA),Pascal Shelutete akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari na Wana habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano
wa mwaka huu ni “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”.
Uongozi wa juu wa TANAPA wakiwa katika picha ya pamoja na Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali.
Uongozi wa juu wa TANAPA wakiwa katika picha ya pamoja
0 comments:
Post a Comment