Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Mfalme Mswatti wa Swaziland, muda
mfupi kabla ya kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa Marais na
Wakuu wa Nchi za Afrika (AU) unaofanyika Sandton International Conference Center huko
Johanessburg Afrika Kusini tarehe 14.6.2015. Aliyesimama kulia ni Mke wa Rais wa Afrika Kusini Mama Tobeka Madiba Zuma.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Antoinette Sessou Nguesso Mke wa Rais Dennis Sessou Nguesso wa
Congo Brazaville wakati wa sherehe za Ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa Marais na
Wakuu wa Nchi za Afrika unaofanyika
Afrika Kusini tarehe 14.6.2015.
Baadhi ya
wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika wakibadilishana mawazo muda mfupi
kabla ya kuhudhuria kikao cha ufunguzi tarehe 14.6.2015. Aliyekaa katikati ni
Mke wa Rais wa Congo Brazaville Mama Antoinette Sessou Nguesso na kulia ni Mke
wa Rais Afrika Kusini Mama Tobeka Madiba Zuma.
Mke wa Rais
akisalimiana na Madame Monica Geingob, Mke wa Rais wa Namibia wakati wakisubiri
ufunguzi rasmi wa mkutano wa 25 wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika
unaofanyika huko Afrika Kusini.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akimsalimia Mke wa Rais wa Kenya Mama Magreth Kenyatta
wakati wa kikao cha Marais na wakuu wan chi za Afrika.




0 comments:
Post a Comment