WATU 23 wamefariki papo hapo huku wengine 34 wakijeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka wakati likijaribu kuyapita magari mengine katika kijiji cha Kinyanambo A, Wilayani Mafundi mkoani Iringa.
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:45 Juni 14,2015, wakati basi hilo likienda Njombe kutokea Iringa katika barabara kuu ya Iringa - Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Pudenciana Protace ameiambia Father Kidevu kwa njia ya Simu kuwa, magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni Lori aina ya Scania lenye namba za usajili T916 AQM lililokuwa na tela T965 BEH Mali ya kampuni ya Bravo Logistic ya jijini Dar es Salaam na basi aina ya Fuso lenye namba za usajili T927 CEF la kampuni ya Another G.
Kamanda ACP Protace amesema madereva wote wawili wa magari hayo, Nicholaus Nagura (30) mkazi wa Makambako aliyekuwa akiendasha basi na Rogers Wales 'Mdue' (35) mkazi wa Mwanza aliyekuwa akliendesha lori wote wamefariki.
Aidha amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi aliyekuwa akiyapita magari mengine kisha basi hilo kuligonga kwa ubavuni lori hilo na kupinduka.
Alisema kuwa kati ya watu hao 23 waliopoteza maisha wanaume ni 16 wakiwapo watoto 3 na wanawake ni 7. huku majeruhi hao 34 wanaume ni 18 na wanawake ni 16 na kati yao watoto wakike ni 2.
Kamanda ACP Protace amesema hali za majeruhi 30 zinaendelea vizuri ila 4 hali zao ni mbaya.

0 comments:
Post a Comment