Mwenyekiti wa CCM
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu Mwenyekiti Zanzibar ambaye pia ni Rais
wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein(kushoto), Makamu Mwenyekiti Bara Ndugu Philip
Mangula(kulia) na katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana(watatu kushoto) wakati
ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kinachofanyika
katika ukumbi wa White House Mjini Dodoma.
***********
Kamati Kuu imepokea na kutafakari taarifa ya Kamati ya Usalama na
Maadili ambayo ilipitia adhabu waliyopewa wanachama sita waliokiuka
kanuni za Maadili na kupewa Onyo Kali, adhabu iliyodumu kwa kipindi
kisichopungua miezi 12.
Wanachama hao sita ni;-
i. January Makamba
ii. Willium Ngeleja
iii. Steven Wasira
iv. Bernard Membe
v. Edward Lowassa
vi. Fredrick Sumaye
Kamati Kuu imepokea na kukubali pendekezo la Kamati ya Usalama na Maadili ya kumalizaka kwa kipindi cha adhabu kwa wanachama hawa. Kwahiyo adhabu hiyo kwa sasa imemalizika, na wanachama hao wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao katika Chama.
Hata hivyo Kamati Kuu inawataka wanachama hawa na wale wengine wenye nia ya kugombea Urais kupitia CCM Kuzisoma , Kuziheshimu na Kuzizingatia Kanuni za Maadili za CCM na kanuni zingine zinazoongoza mchakato ndani ya Chama, ili wasikumbwe na adhabu itokanayo na kuzivunja kanuni hizo.
Wale wote wanaotaka kugombea, yaani waliokuwa kwenye adhabu na wengine watakaojiingiza kwenye kampeni mapema na hivyo kukiuka maadili na miiko ya Chama, taarifa za kukiuka kwao zitatumiwa wakati wa kuchuja majina ya wagombea utakapofika.
Taarifa hizo zitatumika katika kuwapima na kuamua iwapo wana sifa za kutosha na wanafaa au hawafai katika kupata uteuzi wa nafasi wanayoiomba.

0 comments:
Post a Comment