Napenda kuanza porojo zangu hii leo kwa kuweza
wazi kuwa nina maslahi makubwa sana na jambo ambalo leo naenda kulipigia
porojo.
Ndio nina maslahi maana mimi ni mkazi wa
Bombambili Kivule jijini Dar es salaam na barabara ya Ukonga Mazizini - Moshi Bar
– Kwa Mkolemba au Moshi Bar kwa Diwani – Bombambili ndizo barabara zangu
nipitazo kila siku.
Tulilia wakazi wa Ukonga Mazizini kwa muda mrefu
juu ya kusahaulika kwa barabara yetu na hatimaye Mungu alisikia kilio chetu
tukapatiwa kalami kiduchu kuanzia Mombasa hadi Zahanati pale Transfoma.
Kilio kikabaki wa kipande kingine sasa kuanzia
hapo Mazizini hadi Moshi bar – Kwa Mkolemba na Moshi Bar Bombambili kupitia kwa
Diwani.
Barabara hii ilijaa mahandaki na si mashimo
jambo ambalo lilisababisha watumiaji sisi wa barabara hiyo kutafuta njia za
panya kupita katikakati ya makazi ya watu.
Mwaka huu baada ya kukatika kwa mvua ambazo
ziliharibu vilivyo miundombinu ya barabara hizi nilizotaja hapa juu palianza
kujengwa kwa kuchongwa na kisha baadhi ya maeneo kumwagwa kifusi.
Hilo lilitoa faraja sana kwa wakazi wa Ukonga na
vitongoji vyake, mnamo mwezi Julai tarehe 22 kam sijakosea, Mstahiki Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa na viongozi mbali mbali akiwepo
Diwani wa kata ya Ukonga, Elizabeth
Mbano na Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu walitembelea
barabara hiyo kuakagua ujenzi wake.
Picha zilipigwa wakati wa tukio hilo na Blog hii
ilizichapisha maana hata ubovu wa awali ilichapicha sana picha za ubovu huo na
mahandaki yaliyopo.
Meya Silaa ambaye ni mkazi na Diwani wa Gongo la
Mboto eneo jirani na Ukonga alizungumza na wanchi wachache waliofika kumlaki.
Miongoni mwa vitu alivyo sema siku hiyo ni
pamoja na gharama za ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 3 ambapo
alisema itagarimu Milioni 90 na itajengwa kwa kiwangio cha Changarawe na pia
fedha hizo ni za ndani ya Manispaa hakuna mkono wa wahisani.
Porojo zangu hii leo ni shaka niliyonayo juu ya
ujenzi ule wa kiwango cha Changarawe! Na sijui ilikuwa ni kufukia tu maeneo
korofi au kuchonga na kuweka kifusi kwa urefu huo wa kilometa 3?
Maana tunacho kiona watumiaji wa barabara ile ni
vumbi tu na mashimo kurudi pale pale maana kiukweli hakuna kilicho fanyika na
fedha zetu wananchi wa manispaa ya Ilala tunaweza kusema zimeliwa au tumepigwa
vumbi la uso.
Meya Silaa nui ndugu yangu na jamaa yangu sana
lakini nasema wazi kilichofanyika katika barabara hii ni aibu kwa uongozi wako
makini na ni dhihaka kwa wakazi wa Ukonga na vitongoji vyake.
Barabara ya kwa Diwani ilikuwa sio mbaya awali
kama ilivyo sasa lakini baada ya tinga tinga la mkandarasi Yule kupita
liliharibu kabisa njia ile na mvua zikichanganyia ni kilio.
Milioni 90 kutumika kwa kuweka vifusi viwili
vitatu bila kuweka hata makalavati mawili matatu katika maeneo ambayo yalikuwa
na mkondo wa maji imeshindwa?
Lakini hebu Mhandisi wa Manispaa ona aibu na
wewe, ulikuja kweli kukagua ujenzi ule au ndio kumwamini mkandarasi kupita
kiasi.
Naamini bado ni mapema sana wahusika ambao
mlikuja mazizini kukagua ujenzi ule mkandarasi alipoanza basi mfike na leo muangalie
na mpite maeneo yote ya barabara mpate kujionea milioni 90 zilivyotumika.
Fedha hizo hata wangepewa wananchi wajitokeze na
majembe na sepeto zao walahi isingejengwa kwa kiwago kile.
Huu ni utumiaji mbaya wa fedha za wananchi hivyo
hauna budi kuangaliwa.
asante baba, bahati mbaya Magufuri Pombe ni wa Tanroads peke yake tungemuomba awaulizie. Ila nadhani wananchi bila kuvunja sheria ya KUANDAMANA, chagueni wajumbe waende kwa Meya wa Ilala wamuulize USO/USO, ndiyo jibu litapatikana kuandika yanaishia hapa. Poleni sana. Hii ni Dunia ya pili kutoka mwisho. Maneno mengi bila vitendo.
ReplyDelete