Mtoto Colins Silvanus Mzeru
mkazi wa Tabata Dar es Salaam, akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam
jana alipofika na mamayake mlezi, Nora Mzeru kukanusha tuhuma dhid i ya mamayake
huyo kuwa amemfungia na kumtesa kwa muda mrefu sasa na kushindwa kwenda shule.
Colins amesema mama yake huyo
mlezi hana tatizo nae na amekuwa akiishi nae kwa muda mrefu sasa vizuri tangu
kufariki kwa mama yake mzazi na yeye kuchukuliwa na baba yake na kupokelewa bna
mama yake huyo aliyekuwa akiishi na baba yake na kulelewa vizuri hadi sasa
licha ya kuwa baba yake mzazi nae kufariki.
Bi Nora Mzeru ambaye ni Mwenyekiti
wa UWT wilaya ya Ilala amekanusha vikali taarifa zilizokuwa zikirushwa na Kituo
kimoja cha Redio maarufu jijini Dar es Salaam juu ya kuteswa kwa mtoto huyo na
kudai kuwa wanaofanya hivyo wanalenga
kumchafua na ambapo amesema wanaofanya hivyo ni mama wadogo na wajomba wa
Colins ambao wameanza kufanya hivyo tangu kufariki kwa mumewe.
0 comments:
Post a Comment