Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam leo juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaotaraji kuanza leo katika ukumbi wa Karimjee na kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete kesho kutwa.
Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam jana juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaofanyika ukumbi wa Karimjee. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Amantius Msole, wabunge wa EALA kutoka Tanzania Twaha Taslima na Shy Rose Banji
Ndugu Waandishi wa Habari,
Napenda kuwakaribisha wote kwenye mkutano huu wa waandishi wa habari ulioitishwa ili kuwafahamisha kuhusu mkutano wa kwanza wa kikao cha tatu cha Bunge la Tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) unaonza tarehe 27 Agosti 2014 mpaka tarehe 5 Septemba 2014 kwenye ukumbi wa Karimjee hapa jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Wabunge kutoka Tanzania, Adam Kimbisa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam leo, juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaofanyika ukumbi wa Karimjee. Kushoto ni Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa,wabunge wa EALA kutoka Tanzania, Twaha Taslima na Shy Rose Banji.
Mbunge wa EALA kutoka Tanzania, Twaha Taslima akizungumza na wabunge wenzake.
Mkutano ukiendelea
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Amantius Msole akifafanua jambo. Kulia ni Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa
Wanahabari wakichukua dondoo za mkutano huo.
Mbunge Shy Rose Banji akifafanua jambo
Wabunge wakibadilishana mawazo baada ya kumaliza kwa mkutano huo ambapo walisifu kupata idadi kubwa ya waandishi kuliko nchi nyingine.
Ofisa wa Bunge la Tanzania Prosper Minja (katikati) akizungumza jambo na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki Adam Kimbisa (kulia) na Angela Kiziga.
Wabunge wakitoka nje ya chumba cha mkutano.
********
MKUTANO WA KWANZA – KIKAO CHA TATU – BUNGE LA TATU
(IMETOLEWA NA MH. (Dk.) MARGARET NANTONGO ZZIWA – SPIKA,
EALA)
Ndugu Waandishi wa Habari,
Napenda kuwakaribisha wote kwenye mkutano huu wa waandishi wa habari ulioitishwa ili kuwafahamisha kuhusu mkutano wa kwanza wa kikao cha tatu cha Bunge la Tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) unaonza tarehe 27 Agosti 2014 mpaka tarehe 5 Septemba 2014 kwenye ukumbi wa Karimjee hapa jijini Dar es Salaam.
Kwa niaba ya Bunge la EALA na kwa niaba
yangu mimi binafsi, napenda kutoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais Dk.
Jakaya Mrisho Kikwete, na Serikali nzima ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
kwa kukubali kuwa mwenyeji wa EALA kwenye nchi hii kubwa na kwa kukubali
kutufungulia rasmi mkutano wetu.
Tunatoa shukrani za pekee kwa uongozi mahiri
wa Mheshimiwa Dk. Kikwete kwa nchi ya Tanzania na vilevile kwa mchango wake kwa
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kama mwanachama wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi
wa Jumuiya hii (Summit).
Hii
ni mara ya kwanza kwa Bunge la Tatu kufanya mkutano wake Dar es Salaam, ikiwa
ni sehemu ya utaratibu wetu mahsusi tuliojiwekea wa kufanya vikao kwa zamu
kwenye nchi zote wanachama ili kuliweka Bunge hili liwe karibu zaidi na
wananchi ili wapate fursa kufahamu kuhusu shughuli za EALA. Vikao vya Bunge
hili sasa hufanyika mara kwa mara kwenye nchi wanachama kwa mujibu wa Ibara ya
55 ya Mkataba (Treaty) wa uanzishwaji
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Tunapenda kumshukuru mwenyeji wetu, Spika wa
Bunge la Tanzania, Mh. Anna Makinda, kwa kutupa nafasi ya kutumia nyenzo za
Bunge la Tanzania na ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya mkutano wetu. Hii
inaendelea kudhihirisha uwepo wa mahusiano ya karibu ya kikazi kati ya Bunge la
Tanzania na EALA.
Katika kipindi kijacho cha wiki mbili, ratiba
ya shughuli za kazi za Bunge la EALA ni kama ifuatavyo:
·
Ufunguzi
rasmi wa mkutano wa Bunge na Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete;
·
Kupokea na kujadili ripoti kutoka Kamati mbalimbali za Bunge. Ripoti
hizi ni pamoja na ya Kamati ya Masuala ya Jumuiya na Upatanishi wa Migogoro (Committee on Regional Affairs and Conflict
Resolutions) and Kituo cha Uongozi cha Afrika cha Taasisi za Afrika
Mashariki na Usalama wa Jumuiya (African
Leadership Centre on East African Societies and Regional Security); Ripoti
ya Kamati ya Kilimo, Utalii na Maliasili (Committee
on Agriculture, Tourism and Natural Resources) kuhusu semina ya Wabunge wa
Jumuiya juu ya Misitu na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Ripoti ya Kamati ya
Mawasiliano, Biashara na Uwekezaji (Committee
on Communication, Trade and Investment) kuhusu Sekta ya Urafiri wa Anga ya EAC.
·
Aidha, kuna Miswada kadhaa ambayo iko mbele ya Kamati mbalimbali
za Bunge. Hii ni pamoja na:
a) Muswada
wa Elimu -- the EAC Integration (Education) Bill – ambapo Bunge linatarajia kupokea
taarifa kutoka Kamati ya Masuala ya Jumuiya na Upatanishi wa Migogoro (Committee on Regional Affairs and Conflict
Resolution) kuhusu hatua waliofikia;
b) Muswada
wa Masuala ya Ushirika -- the EAC
Co-operatives Societies Bill – huu uko mbele ya Kamati ya Kilimo, Utalii na
Maliasili (Committee on Agriculture,
Tourism and Natural Resources), ambayo hivi karibuni inatarajiwa kuanza
vikao vya wazi;
c) Muswada
wa Masuala ya Biashara -- the EAC Joint Trade Negotiations (Repeal) Bill – ambao
uko mbele ya Kamati ya Mawasiliano, Biashara na Uwekezaji (Committee on Communication, Trade and Investments).
·
Hatimaye, Bunge la EALA litapitia Hoja, Maazimio na Maswali
mbalimbali ambayo yatakuwa yameletwa kwenye mkutano.
Kwa ujumla, EALA inatoa mchango wake kwenye
mchakato wa utengamano kwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na mfumo rasmi wa kisheria
na usimamizi ili kuwepo na kipaumbele
kwa ajenda ya utengamano.
Ni muhimu kuhakikisha kuwa wananchi wa
Afrika Mashariki wanahusishwa kwenye mchakato huu. Kama EALA tutaendelea kuwa
karibu na wananchi wa Jumuiya hii na kuhakikisha kuwa maoni yao yanasikilizwa
wakati wa kutunga Sheria.
Siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita, EALA
ilifanya ziara mahsusi kwenye vyombo vya habari vya IPP Media jijini Dar es
Salaam na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni hayo, Dk.
Reginald Mengi. Tunapenda kutoa shukrani kwa IPP Media kwa kuamua kutuunga
mkono kwenye urushwaji wa moja kwa moja (live
broadcast) wa ufunguzi rasmi wa mkutano wa Bunge letu. Hii ni hatua ya
kwanza ya jitihada zetu za kuhakikisha kuwa tunajenga mahusiano ya karibu kati
ya vyombo vya habari na Wabunge wa EALA ili tuweze kutangaza ajenda ya
utengamano na kuelimisha wananchi kuhusu majukumu ya Bunge letu. Tutaendelea
kufanya majadiliano haya na vyombo vya habari vingine kwenye nchi zote
wanachana wa EAC.
Taasisi nyingine ambazo
tutazitembelea wakati wa kikao chetu ni pamoja na Mamlaka ya Bandari ya
Tanzania (TPA) mnamo tarehe 29 Agosti 2014, na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TASUBA)
iliyopo Bagamoyo tarehe 30 Agosti 2014. Ziara hizi zinatarajia kuongeza
ushirikiano kati ya EALA na washikadau husika kwa upande mmoja na kuboresha
kazi zetu za utungaji wa sheria kwa upande mwingine.
Jumuiya ya EAC hivi sasa inapitia katika
kipindi muhimu cha mchakato wa utengamano. Tunatoa pongezi kwa nchi zote
wanachama kwa kuonesha moyo wa dhati wa kuimarisha mchakato wa utengamano kwa
kutekeleza Itifaki mbalimbali.
Umoja wa Forodha (Customs Union) sasa uko kwenye hatua nzuri ya utekelezaji. Ndani ya
umoja huu, bidhaa zinazozalishwa kwenye Jumuiya hazitozwi kodi na nchi
wanachama na zinafaidika na kodi sawasawa ya nje, pamoja na utaratibu na
nyaraka za pamoja. Kuanzishwa kwa Himaya Moja ya Forodha (Single Customs Territory) ni jambo jingine kubwa kwenye EAC, kwani
kutawezesha bidhaa ziweze kusafiri kwa kasi zaidi. Lengo la kuwa na Himaya Moja ya Forodha ni kuhakikisha
kuwa nchi wanachana zinanufaika kwa pamoja kwa kuunganisha uchumi wa nchi hizi
kwa lengo la kuunga mkono jitihada za maendeleo ya uchumi.
Mwaka wa nne wa utekelezaji wa Soko la
Pamoja umeanza. Itifaki ya Soko la Pamoja (Common
Market Protocol) inahakikisha kuwa kunakuwa hakuna vikwazo vyovyote kwa
bidhaa, huduma, ajira, mitaji na uanzishaji wa biashara miongoni mwa wananchi
wa nchi wanachana wa Jumuiya. Kwa ujumla, nchi wanachama zimeonesha utashi mkubwa
wa kusimamia utekelezaji wa Itifaki hii. Jumuiya ya EAC pia imesaini Itifaki ya
kuanzisha Umoja wa Fedha (Monetary Union),
ambayo ni hatua ya tatu muhimu kwenye mchakato wa utengemano ambao unapitia
kwenye hatua kubwa nne.
Nimetaarifiwa kuwa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania tayari imeshatia saini kupitisha Itifaki ya Umoja wa Fedha (Monetary Union Protocol).
Utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Fedha
unatarajia kuanza mara baada ya nchi zote wanachama kuidhinisha itifaki hiyo na
kukabidhi nyaraka hizo kwenye ofisi ya Katibu Mkuu wa EAC. Hii ni hatua muhimu
sana ambayo itasimika mchakato huu wa utengamano. Hata hivyo, utekelezaji rasmi
wa Itifaki hii utahitaji kuwepo kwa sheria mbalimbali. Kama EALA, tumejidhatiti
kuhakikisha kuwa tunatunga sheria hizi na hapa tungependa kutoa wito kwa Baraza
la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Council
of Ministers) kuleta hii Miswada kwenye Bunge haraka iwezekanavyo.
Pamoja na hatua hizi kubwa ambazo tumepiga,
bado kuna changamoto. Kama ilivyoelezwa awali, hatuna budi kuhakikisha kuwa vikwazo
vya kibiasha visivyo vya kiforodha (Non-Tariff
Barriers) vinashughulikiwa kikamilifu. Utaratibu mahsusi ni lazima uwekwe
na utekelezwe kuondoa hivi vikwazo na kama EALA tutatoa wito kwa Kikao cha
Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (Summit) kuharakisha mchakato huu. Changamoto nyingine ni pamoja na
kusuasua kwenye utekelezaji wa ajenda ya EAC kwenye sera za taifa za nchi
wanachama wa Jumuiya. Tutaendelea kushirikiana na Baraza la Mawaziri la Jumuiya
ya Afrika Mashariki na washikadau wengine kutimiza wajibu wetu kama
ilivyoainishwa kwenye Mkataba ili kuhakikisha kuwa Jumuiya yetu ya kiuchumi
inatengemaa.
Ni muhimu kuzingatia kuwa sheria ambazo
zinapitishwa na EALA kwa niaba ya EAC zina nguvu ya kisheria na zinatakiwa
kupewa kipaumbele kuliko sheria nyingine zilizopo kwenye nchi wanachana
kuhusiana na masuala ya Jumuiya. Hivyo basi, tunatoa wito kwa nchi zote
wanachama kuharakisha mchakato wa kuhakikisha kuwa sheria za nchi zao zinaoanishwa
ili ziweze kuendana na sheria za Jumuiya.
Napenda kutoa wito kwa vyombo vya habari
vyote kuwa vishirikiane na EALA katika kutangaza vikao vya Bunge letu katika
kipindi hiki cha wiki mbili ambapo tutakuwa tunakutana Dar es Salaam.
Nawashukuru sana kwa kunisikiliza.
0 comments:
Post a Comment