Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete (aliyenyoosha mkono),
akimuonyesha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana mandahari ya eneo la
Ziwa Tanganyika, linalotumiwa na wavuvi katika eneo la Kabwe wilayani
Nkasi mkoani humo, Kinana alipokuwa katika ziara ya kukagua utekelezaji
wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia ya
kuzitatua katika eneo hilo la Wavuvi, leo.
Katibu Mkuu wa CCM akitazama eneo la uvuvi katika ziawa Tanganyika, kwenye eneo la Kabwe mkoani Rukwa leo
Mfanyabiashara
ya kusafirisha na kusindika samaki kutoka ziwa Tanganyika, Mohamed
Shibibi (wapili kushoto) akimpatia maelezo Katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Kinana jinsi anavyohifadhi samaki katika majokofu baada ya
kuvuliwa, Kinana alipokagua shughuli za mfanyabiashara huyo, kwenye eneo
la wavuvi wa Kata ya Kabwe, wilayani Kansi mkoani Rukwa leo. Kushoto ni
Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume.
Kinana akitazama lundo la samaki aina ya migebuka kwenye kituo cha wavuvi cha Kabwe, katika ziwa Tanganyika
Wananchi
wa Kabwe, wakiwa wamebeba samaki mkubwa kutoka Ziwa Tanganyika, wakati
Kinana na Mbunge wa Nkasi Kaskazini Ali Kessy wakiwafuata kwa nyumba
baada ya kutoka kukagua shughuli za wavuvi katika eneo lawafugaji la
Kabwe mkoani Rukwa.
Mkurugenzi
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Makao Makuu ya CCM, Godfrey
Chongolo, akiwa na kina mama waliokuwa wakikunja samaki aina ya migebuka
katika mwambao wa ziwa Tanganyika eneo la Kabwe, Wilayani Nkasi mkoani
Rukwa.
0 comments:
Post a Comment