Nafasi Ya Matangazo

March 12, 2014



WAKATI uchaguzi wa Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge Maalumu la Katiba ukitarajiwa kufanyika leo, wagombea wawili waliojitokeza kutaka kuwania nafasi hiyo, wameenguliwa baada ya ya kushindwa kurudisha fomu ya kuwania nafasi hiyo kwa muda uliopangwa

Wajumbe hoa Dk Theria Uvisa pamoja na Danstan Chipaka walienguliwa katika kinyang’anyiro hicho kufuatia kushindwa kurudisha fomu za kugombea ambazo zilipaswa kurudishwa leo saa 4 asubuhi.

Kufuatia kuenguliwa kwa wajumbe hao, nafasi hiyo itawaniwa na Samwel Sitta pamoja  na Hashim Rungwe ambao ndiyo waliokidhi vigezo kwa kuchukua fomu na kurudisha kwa wakati.

Uchaguzi wa Mwenyekiti unatarajiwa kufanyika leo saa 10 jioni, ambapo baada ya kutangazwa matokeo kutatangazwa uchukuaji fomu kwa wajumbe watakaotaka kuwania nafgasi ya umakamo mwenyekiti.

Mpaka sasa anayetajwa kutarajiwa kuwania nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti, ni Samia Suruhu.

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Makamu Mwenyekiti wa Bunge anapaswa kutoka upande wapili wa muungano iwapo Mwenyekiti atakuwa amechaguliwa kutoka upande mwingine wa muungano hili kuleta usawa.
Posted by MROKI On Wednesday, March 12, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo