Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa PSPF, Adam Mayingu akizungumza na Waandishi wa
habari pamoja na wadau wa mfuko huo katika semina ya siku moja kuhusu
shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo na fursa mbalimbali pamoja
na mafao yanayotolewa na mfuko.
Miongoni mwa huduma wanazotoa na ikiwa ni huduma ya fao jipya ni Mpango wa Uchangiaji kwa Hiyari (PSS) ambapo mwanachama anatakiwa kujiunga kwa kiwango cha chini cha shilingi 10,000/= na kuchangia kadri awezavyo kila siku, wiki, Mwezi na kwa msimu kadri uwerzavyo. Semina hiyo imefanyika katika ukumbi
wa JB Belmont Hotel jengo la Golden Jubilee Towers jijini Dar es Salaam.
Neema Muro Mkurugenzi wa Uendeshaji katika mfuko huo akitoa mada juu ya uwekezaji katika mfuko wa PSPF.
Mkurugenzi
wa Fedha Masha Mushomba akizungumzia masuala ya fedha na ukusanyaji
pamoja na ulipaji mafao kwa wanachama wa mfuko huo.Andrew Nkangaa Mkurugenzi wa Tehama katika mfuko huo akizungumzia jinsi wanachama wanavyoweza kuchangia mfuko huo kwa kutumia mitandao ya simu na kurahisisha shughuli zao za kila siku badala ya kufuata ofisi za PSPF zilipo kwa ajili ya kwasilisha michango yao.
Wanahabari ambao ni washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakifuatilia mada kwa umakini. Bloggers Shamim Mwasha wa 8020 Fashion Blog, na John Bukuku wa Fullshangwe Blog wakifuatilia mada pamoja na Sauda (kulia) kutoka EATV na Radei 5.
Wachora katuni wao waliendelea kusikiliza huku wakichora vibonzo vyao. Wanahabari walisikiliza kwa umakini mkubwa kila kilichoelezwa na viongozi wa PSPF.
Meneja Mawasiliano na Masoko wa PSPF, Costantina Martin ndio alikuwa Mc wa Semina hiyo ama mchombezaji.
Hizi ni huduma mbalimbali zitolewazo na PSPF
Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Gabriel Silayo nae aleelezea mikakati ya PSPF.
Washiriki wa semina walimsikiliza Silayo vyema.
Mwanahabari mkongwe, Deogratius Mushi akisema neno la shujkrani kutokana na kile alichokipata wa niaba ya washiriki wote.
0 comments:
Post a Comment