Redds Miss Lake
zone 2012/13 Eugene Fabian (katikati) akiwa pamoja na , mshindi wa Tatu
Happiness Rweyemamu na Kulia kwake ni mshindi wa pili Happiness Daniel warembo
hawa wataingia kambi ya REDDS Miss Tanzania 2012.
******
Jumla ya warembo
30 wanataraji kuingia kambi ya REDDS MISS TANZANIA 2012 wakati wowote baada ya
kumalizika kwa mashindano ya Vitongoji, Mikoa, na hatimaye Kanda mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa
mashindano hayo ya Kanda ambayo kila Kanda imetoa washindi wa tatu ambao
wataziwakilisha Kanda zaoi katika Shindano hilo kubwa na laiana yake.
Warembo
hao na Kanda zao wanazotoka ni Redds Miss Kanda ya Kaskazini Warida Frenk, Anande Raziel na Lucy Stefano,
Redd’s
Miss Kanda ya Mashariki 2012 ni Rose
Lucas, Irine Veda na Joyce Baluhi , Redds
Miss Kinondoni Brigit Alfred, Diana George Hussein na Irene David.
Kanda
nyingine ni Redds Miss Lake zone 2012 Eugene Fabian,Happiness Daniel na Happiness
Rweyemamu, Redd's Miss Tameke 2012, Edda Sylvester, Flavian Maeda na Catherine
Masumbigana, Redds Miss Kanda ya Kati, Belinda Mbogo, Lightness Michael na Elizabeth
Diamond.
Washiriki
wengine watakao ingia Kambini ni kutoka kanda ya Redds Miss Ilala 2012, Mary Chizi, Magdalena Munisi na Noela
Michael, Redds Kanda Vyuo
vya Elimu ya Juu, Virginia Mokiri, Fatma Ramadhani na Fina Revocatus, kanda
nyingine ni ya Kutoka Chuo Kikuu Huria ni Zuwena Nassibu na Redds Miss Southern Zone Naomi Jones, Caren Elias na
Venance Edward.
Kesho Septemba 26, 2012 Kamati ya Miss Tanzaniaikiongozwa
na Mkurugenzi wake Hashim Lundenga kutoka Lino International Agency watakutana
na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maeleo majira ya saa
4:00 asubuhi kuzungumzia maandalizi ya Kambi hiyo.
Redds Miss
kanda ya Kaskazini Warida Frenk katikati akiwa na washindi wenzake Anande
Raziel kulia na lucy stefano kushoto mara baada ya kutawazwa kuwa washindi wa
Redds Miss Kanda ya kaskazini,Washindi hao wanatarajiwa kujiunga kwenye kambi
ya Redds Miss Tanzania hapo baadae ili kujiandaa na shindano la Taifa la Redds
Miss Tanzania.
Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012,
Rose Lucas katikati akipunga mkono kwa furaha akiwa na mashindi wa pili Irine
Veda (kulia) na Mshindi wa tatu Joyce Baluhi mara baada ya warembo hao
kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo lililofanyika mjini Morogoro usiku wa
Septemba Septemba 1, mwaka huu. Warembo hawa wote watashiriki shindano la
Redd’s Miss Tanzania 2012 baadae mwaka huu.
Mshindi wa shindano la Redds Miss
Kinondoni Brigit Alfred, akiwapungia mkono mashabiki walioshuhudia shindano
hilo jijini Dar es Salaam jana, kulia ni mshindi wa pili Diana George Hussein
na mshindi watatu Irene David. Brigit pia anashikilia taji la Redds Miss Sinza
2012 huku Irine akishikilia taji la Miss Ubungo 2012.
Malkia wa Redd's
Miss Tameke 2012, Edda Sylvester (katikati), akiwa na mshindi wa pili Flavian
Maeda (kushoto), pamoja na Catherine Masumbigana aliyeshika nafasi ya tatu
katika kilele cha mashindano hayo, Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam usiku
wa kuamkia leo.
Naomi Jones, Caren Elias na Venance
Edward
Redds Miss Kanda
ya Kati, Belinda Mbogo (katikati) akiwa na mshindi wa pili Lightness Michael
(kushoto) na mrembo aliyetwaa nafasi ya tatu Elizabeth Diamond baada ya
kumalizika kwa shindano hilo mjini Dodoma hivi karibuni. warembo hawa wote
wameingia kambi ya Miss Tanzania 2012.
Redds Miss Ilala 2012,
Noela Michael akiwa na mshindi wa pili Magdalena Munisi (kulia) na mshindi wa
tatu Mary Chizi (kushoto) mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la
Redd's Miss Ilala 2012.
0 comments:
Post a Comment