Nafasi Ya Matangazo

May 04, 2017

Kila ifikapo jioni majira ya saa 10 hivi, baadhi ya wakazi wa Moshi wanakuwa katika haraka ya kwenda mahali kujipatia chakula wakipendacho. Chakula hiki kimetokea kuwavuta wengi sana ambao hata hapo awali walikuwa wakiamini yakwamba ulaji wa mihogo ni hatari sana.

Hofu hii ilitokana na baadhi ya wenyeji wa Mkoa wa Kilimanjaro hususani wachagga kuamini kuwa mihogo ni sumu na si chakula, lakini siku hizi mihogo inalika kwa wingi katika mji huu bila kuchagua kabila la mchagga, mpare, muarusha, mzungu ama anatoa Esia. 
Aliyefanikiwa kuwateka wakazi wa Moshi na kuwafanya kila ifikapo jioni wahahe kuitafuta Mihogo si mwingine bali ni Mzaramo Mzaliwa wa Chanika pale Kisumu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na hapa moshi anajulikana kama Mzee Kajembe. 
Nilipofika katika ofisi yake swali la kwanza kumuuliza kuwa “Mzee wewe ni mwenyeji wa wapi?” akiwa na tabasamu na pasi na shaka alinijibu kuwa mimi mwenyeji wa jiji la Dar es Salaam.
Kwajibu hilo, nikawa sina swali bali nilimpa hongera kwa kufanikiwa kuleta chakula cha Kizaramo mjini Moshi na kukiandaa vyema kiasi cha Mchagga kushindwa kulala bila kula kipande cha Mhogo kutoka kwa Kajembe.

Jinalake halini ni Rashid Nassor Kajembe, ananiambia kuwa aliingia mji wa Moshi akiyoka uzaramkoni mwaka 1982 na ilipofika mwaka 1984 akaamua kuanza kuuza mihogo ya kukaanga. 

Anasema mwanzo daima ni mgumu lakini sasa kidogo afadhali, maana anasema alipoanzia DSM Street miaka hiyo na bade katika mitaa ya Simu tofauti na sasa alipo New Street.

Kiukweli anawateja wa kila namna anasema Wahindi nao wanaila sana mihogo tena huifuata na kupanga foleni. Mhindi anasema “Walahi Ogo tamu kushinda Makate” Tupate matukio zaidi ya picha.
 Mihogo ikiwa jikoni katika eneo ambalo Mzee Kajembe anafanyia biashara Kajembe Shop.
 Kajembe akiwa na kijana wake Juma Kajembe wakimenya mihogo majira ya asubuhi.
  Mzee Kajembe akimenya mihogo hiyo
Wateja wa Mihogo ya Mzee Kajembe kama nilivyowaambia hapo awali kuwa ni wa kila aina na kila rika.
 Mmoja wa vijana wa Mzee Kajembe, Mohamed Ally akiweka mihogo jikoni

 Vijana hawapendi Chips mjini Moshi ni Mihogo tu kutoka kwa Mzee Kajembe
 Mdau nakusihi ufikapo mjini Moshi usiache kufika New Street jirani na Hoteli maarufu za Zebra na Buffalo ujipatie Mihogo ya aina yake.
Posted by MROKI On Thursday, May 04, 2017 4 comments

4 comments:

  1. wow jamaniiiiiiiiiiiii nimemimmiss sana iyo mihogo big up sana kajembe...mungu akuzidishie uzima.

    ReplyDelete
  2. Mroki hivi hujui kazi ya mihogo kwa afya hahahah basi wachaga wamegundua ipo kazi.

    ReplyDelete
  3. Kajembe hana mpinzani kwa suala zima la kukaanga mihogo, pili ni msafi sana

    ReplyDelete
  4. LoL ila hiyo foleni ya mhogo ahaaa ni kazi

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo