Nafasi Ya Matangazo

December 22, 2008

Wizara ya Elimu leo imeatangaza rasmi matokeo ya darasa la saba na kuutaja mkoa wa Shinyanga kuwa wakwanza toka mwisho katika mtihani wa darasa la saba huku Mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza kwa kufanya vizuri.
Katika matokeo hayo, asilimia 80.73 ya wanafunzi 433,260 waliofaulu darasa la saba wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza katika shule za serikali, wakiwamo wasichana 188,460 sawa na asilimia 82.13 na wavulana 244,800 sawa na asilimia 79.69 ya wavulana waliofaulu.
Hata hivyo, ufaulu wa masomo ya Hisabati na Kiingereza uko chini.
Akitangaza matokeo hayo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe (pichani juu) alisema kati ya wanafunzi wote 1,017,967 sawa na asilimia 97.51 ya walioandikishwa, walifanya mtihani huo na wanafunzi 536,672 sawa na asilimia 52.73 wamefaulu.
Katika matokeo hayo ambayo yataanza kutangazwa na kila mkoa leo, wavulana walifanya vizuri zaidi ambapo walikuwa 307,196 sawa na asilimia 59.75 huku wasichana waliofaulu ni 229,476 sawa na asilimia 45.55.
Aliitaja mikoa iliyofanya vibaya na kiwango cha ufaulu kwa asilimia kwenye mabano ni Shinyanga (34), Lindi(40.7), Mara (42.6) na Tabora (43.2).
Kwa mikoa iliyofanya vizuri ni Dar es Salaam (73.9), Arusha (69.2), Iringa (64.1) na Kagera 63.5. Kwa upande wa wanafunzi waliobainika kufanya udanganyifu, alisema “watahiniwa 102 wamefutiwa mitihani wakiwamo wasichana 41 na wavulana 61.”
Habari zaidi kesho soma HabariLeo au ingia hapa www.habarileo.co.tz
Posted by MROKI On Monday, December 22, 2008 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo