Kamishina wa Polisi Jamii, CP Alex Mkama, amewataka Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi kutumia mafunzo waliyoyapata kuboresha utendaji wao wa kazi na kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika tasnia ya habari.
CP Mkama ameyasema hayo wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi kilichofanyika katika Chuo cha Polisi Tanzania, Moshi, kuanzia tarehe 28 hadi 30 Septemba 2026.
Amesema mafunzo waliyoyapata yanapaswa kwenda kufanyiwa kazi kwa vitendo, akiwataka Maafisa Habari hao kuwa wabunifu, hususan katika matumizi ya mitandao ya kijamii, ili kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa haraka na kwa usahihi.
Aidha, amewataka kufanya kazi kwa Nidhamu,Haki, Weledi, na Uadilifu pamoja na uzalendo, huku wakitambua wajibu wao wa kutetea amani ya Jeshi la Polisi na nchi kwa ujumla.
CP Mkama pia amewataka Maafisa Habari hao kuendelea kuboresha utendaji wao katika tasnia ya habari kwa kutumia maarifa waliyoyapata, akisisitiza umuhimu wa kutomwangusha Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.







0 comments:
Post a Comment