Nafasi Ya Matangazo

June 11, 2026






Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mheshimiwa Remidius Mwema, leo tarehe 10 Juni 2026, ameongoza kikao maalum cha Kamati ya Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Babati kilicholenga kujadili na kuratibu maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2026.

Kikao hicho kimewakutanisha viongozi na watendaji kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati (Babati TC) pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Babati (Babati DC), ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa vikao vya maandalizi vinavyoendelea kufanyika kuelekea mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mhe. Mwema amepongeza juhudi na ushirikiano unaoendelea kuoneshwa na halmashauri zote mbili katika maandalizi ya tukio hilo muhimu la kitaifa. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kufanya maandalizi ya kina na kwa wakati ili kuhakikisha shughuli zote zinazohusiana na mbio za Mwenge wa Uhuru zinafanyika kwa ufanisi na mafanikio makubwa katika wilaya nzima.

Kikao hicho ni sehemu ya mfululizo wa mikutano na vikao vya uratibu vinavyoendelea kufanyika kwa lengo la kuhakikisha Wilaya ya Babati inakuwa tayari kupokea na kushiriki kikamilifu katika mbio za Mwenge wa Uhuru 2026
Posted by MROKI On Thursday, June 11, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo