Nafasi Ya Matangazo

April 18, 2026

Uamuzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC),kuongeza safari za treni za SGR kutoka safari mbili  hadi nne kati ya Dar es Salaam na Morogoro si jambo la kawaida tu la ratiba bali ni ishara kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi, kimkakati na kiutendaji.
 
Mosi,  Ongezeko la mahitaji ya abiria (Demand-driven decision), kuongeza safari maana yake ni kwamba, Idadi ya abiria imeongezeka sana na huduma ya SGR imekubalika na wananchi. Kwa mfano, tayari SGR imeonyesha mafanikio makubwa kwa kubeba mamilioni ya abiria na kurahisisha usafiri

Tafsiri yake ni kwamba, TRC haiongezi safari bila sababu bali ni muitikio wake kwa soko.

Pili, Kuboresha upatikanaji wa huduma (Service accessibility), awali safari mbili zilikuwa hazimpi nafasi abiria kuwa na machaguo ya safari   hivyo ilikuwa kwamba

abiria akikosa  treni ya asubuhi ama jioni basi atasubiri muda mrefu.
Kuongeza treni hizo kufikia nne, kunampa machaguo mengi zaidi kwa abiria,  ikiwemo urahisi wa kupanga safari kulingana na muda wa kazi/shughuli husika.

Aidha, hii inaifanya reli, kuwa rafiki kwa wafanyakazi na kuwa  mbadala halisi wa mabasi na magari binafsi

Tatu, kuongezeka kwa ufanisi wa matumizi ya miundombinu, kama inavyofahamika, SGR ni uwekezaji mkubwa wa serikali (mabilioni ya fedha), hivyo kuuongeza safari za treni kati ya Jiji la Dar Es Salaam na Mkoa wa Morgoro, kunamaanisha kwamba, treni zinatumika muda mwingi zaidi na kwamba miundombinu haikai muda mwingi bila kutumika (idle)

Nne, athari chanya kiuchumi, kuwa na Safari nyingi zaidi  ni sawasawa na harakati nyingi zaidi za watu na hii  inasabaisha biashara kuongezeka kati ya Dar es salaam na Morogoro. Aidha ni fursa za ajira (moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja), Ukuaji wa miji, wakati tunaangalia matokeo ya kuongeza treni kati ya maeneo hayo mawili, SGR tayari inachochea biashara, ajira na utalii

Tano,. Kupunguza msongamano wa barabara na gharama za usafiri, kuwa na Safari nyingi za treni kuna maana kubwa sana kufanya barabaara kupumua kwa maana kwamba zinapunguza mabasi barabarani, zinapunguza ajali na uchakavu wa barabara lakini pia zinatoa usafiri wa haraka na wa gharama nafuu. Treni hubeba maelfu ya watu kwa safari moja tofauti na mabasi.

Sita, hatua kuelekea huduma ya “high-frequency rail system”, kuongeza safari ni hatua ya kuelekea mfumo wa kisasa wa reli (kama metro/intercity advanced systems).

Ratiba zinazokaribiana ni ishara kuwa: TRC inaelekea kwenye mfumo wa reli wa kisasa unaofanana na nchi zilizoendelea.
 
Kuongezeka kwa safari kutoka mbili  hadi nne,  kunamaanisha kuwa Mahitaji ya huduma yameongezeka, wananchi wana imani na SGR, uchumi unaanza kunufaika, na huduma inakuwa ya kisasa zaidi na rafiki kwa mtumiaji.


Posted by MROKI On Saturday, April 18, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo