Nafasi Ya Matangazo

January 27, 2026

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, akiwa ameambatana na 
Kamishna wa Fedha na Lojistiki CP Liberatus Sabas, pamoja na maafisa wengine akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, amefanya ukaguzi wa maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi ya askari ambao upo katika hatua mbalimbali za kukamilika.
IGP Wambura, pia amekagua ujenzi wa kituo cha Polisi cha kisasa kitakachokuwa na ghorofa mbili cha wilaya ya Polisi Dodoma ambacho ujenzi wake bado upo katika hatua za awali. Miradi hiyo ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari na kituo cha Polisi Dodoma itarahisisha utendaji kazi wa askari Polisi katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika nchini. Picha na Jeshi la Polisi.
Posted by MROKI On Tuesday, January 27, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo