Nafasi Ya Matangazo

December 13, 2025





Na Mwandishi Wetu, Moshi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw.  Kiseo Nzowa ametoa wito kwa Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) kuweka utaratibu bora kwa ajili ya klabu shiriki kwenye michezo hiyo, kutumia wachezaji kutoka klabu nyingine.

Bw. Nzowa aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa SHIMIWI leo tarehe 12 Desemba, 2025 unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

Amesema kuwekwe kwa mfumo bora unaowatambulisha, kurasimisha na kuruhusu watumishi wachache kutoka sehemu moja wenye vigezo vya kushiriki kwenye michezo ya SHIMIWI katika michezo mbalimbali iliyopo.

“Kama mnakumbuka kipindi cha nyuma chama cha mpira TFF kilikuwa na kanuni isiyoruhusu wachezaji wa nje ya nchi kucheza kwenye ligi ya Tanzania, lakini baadaye walikaa na kubadilisha utaratibu na sasa wachezaji wa nje wanaruhusiwa, hivyo na sisi SHIMIWI tukae tuone njia nzuri yenye mfumo bora wa kuruhusu hawa wanaotoka sehemu nyingine kushiriki bila kuonekana wasiostahili kwa jina la mamluki,” amesisitiza Bw. Nzowa.

Lakini, Bw. Nzowa pamoja na kuonesha changamoto hiyo ya mamluki, lakini amesema SHIMIWI inamafanikio makubwa kwa kufuata kalenda yao kwa kufuata matukio kama yalivyopangwa kuanzia Januari hadi Desemba.
Posted by MROKI On Saturday, December 13, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo