Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza katika Mkutano wa 26 wa Baraza Kuu la Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) Novemba 9, 2025, jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) anayemaliza muda wake, Zurab Pololikashvili akizungumza katika Mkutano wa 26 wa Baraza Kuu la Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) Novemba 9, 2025, jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Baadhi ya wajumbe kutoka nchi mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa 26 wa Baraza Kuu la Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) Novemba 9, 2025, jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) anayemaliza muda wake, Zurab Pololikashvili akizungumza katika Mkutano wa 26 wa Baraza Kuu la Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) Novemba 9, 2025, jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Baadhi ya wajumbe kutoka nchi mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa 26 wa Baraza Kuu la Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) Novemba 9, 2025, jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan
Abbasi, akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 26 wa Baraza Kuu la
Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) kilichoanza leo Novemba 9, 2025, jijini
Riyadh, Saudi Arabia, ameihakikishia dunia kuwa hali ya utalii na amani viko
imara nchini Tanzania kufuatia machafuko yaliyotokea wakati na baada ya
uchaguzi katika baadhi ya maeneo.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo wakati akichangia Taarifa
ya Utekelezaji ya Mwaka ya Taasisi hiyo ambapo pia Tanzania ilinufaika na
programu mbalimbali ikiwemo kuandaa Mkutano wa Dunia Kanda ya Afrika wa Utalii
wa Vyakula uliofanyika Arusha April mwaka huu na kufadhiliwa baadhi ya programu
za utunzaji wa mazingira katika maeneo ya Safu za Milima ya Usambara.
“Mheshimiwa Mwenyekiti wa Baraza hili baada ya kumpongeza
Katibu Mkuu na Sekretarieti ya UN
Tourism kwa utekelezaji ambao Tanzania pia imenufaika, naomba kutumia fursa hii
kutoa taarifa kuwa Tanzania ni salama baada ya kadhia iliyojitokeza wakati wa
uchaguzi.
“Serikali imefanya jitihada na kurejesha nchi yetu katika
hali ya utulivu na hivyo kuendelea kuwa salama kwa watalii na vivutio vyetu
vyote mnavyovijua viko salama. Nawakaribisha wajumbe wa Mkutano huu na wadau
wengine wa utalii kuja na kuendelea
kutembelea nchi hii ambayo ni kivutio bora Afrika kwa utalii wa safari,”
alisema Dkt. Abbasi.
Aidha, mbali ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 32 pekee kati ya wanachama wa Umoja huo
wanaofikia 160 kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji (Executive Committe), leo pia
Baraza Kuu hilo limeipitisha Tanzania kuwa Mjumbe wa Kamati ya Kuhakiki
wanachama (UN Tourism Credentials Committe).
Mkutano huo unaendelea jijini hapa na pamoja na mambo
mengine utajadili kuhusu matumizi ya akili mnemba katika kutangaza utalii na
pia jioni hii umemthibitisha Sheikha Nasser Al Nowais kutoka UAE kuwa Katibu
Mtendaji mpya wa taasisi hiyo muhimu kwa sekta ya utalii duniani.

Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) anayemaliza muda wake Zurab Pololikashvili (wa tano kutoka kushoto mstari wa mbele) katika picha ya pamoja na wajumbe nchi wanachama wa Shirika la Utalii Duniani mara baada ya kufungua Mkutano wa 26 wa Baraza Kuu la Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) Novemba 9, 2025, jijini Riyadh, Saudi Arabia.








0 comments:
Post a Comment