Nafasi Ya Matangazo

October 07, 2025

Afisa Maliasili kutoka Wilaya ya Busega, Bi. Jesca Mathias akizungumza kuhusu taratibu za malipo ya kifuta jasho/machozi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Shigela leo Oktoba 6, 2025 ambapo timu ya wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, TAWA  na Maafisa Wanyamapori wa Halmashauri inaendelea kutoa elimu ya uhifadhi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Shigela wakifuatilia mada mbalimbali kuhusu uhifadhi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Shigela leo Oktoba 6, 2025 ambapo timu ya wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, TAWA  na Maafisa Wanyamapori wa Halmashauri inaendelea kutoa elimu ya uhifadhi Mkoani Simiyu.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Shigela wakifuatilia mada mbalimbali kuhusu uhifadhi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Shigela leo Oktoba 6, 2025 ambapo timu ya wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, TAWA  na Maafisa Wanyamapori wa Halmashauri inaendelea kutoa elimu ya uhifadhi Mkoani Simiyu.

Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Nassoro Wawa akitoa elimu ya uhifadhi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Shigela leo Oktoba 6, 2025 ambapo timu ya wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, TAWA  na Maafisa Wanyamapori wa Halmashauri inaendelea kutoa elimu ya uhifadhi Mkoani Simiyu.
Afisa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Bw. Lusato Masinde akifafanua kuhusu tabia za mnyamapori fisi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Shigela leo Oktoba 6, 2025 ambapo timu ya wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, TAWA na Maafisa Wanyamapori wa Halmashauri inaendelea kutoa elimu ya uhifadhi Mkoani Simiyu.
*************
Na Mwandishi Wetu- Simiyu
Wananchi wa Kijiji cha Shigela Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya fisi wanaovamia makazi ya watu.
 
Rai hiyo imetolewa na Afisa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Bw. Lusato Masinde katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Shigela leo Oktoba 6, 2025 ambapo timu ya wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, TAWA  na Maafisa Wanyamapori wa Halmashauri inaendelea kutoa elimu ya uhifadhi Mkoani Simiyu.
 
"Tuchukue tahadhari kubwa hatuko salama kwa sababu katika mazingira yetu hawa wanyama wapo na kuna vichaka na mapango mengi" amesisitiza  Bw. Masinde.
 
Aidha, amewataka wananchi kuongeza jitihada  katika kuwalinda watoto dhidi ya fisi hao kwa kuwa wao ni waathirika wakubwa.
 
Naye, Afisa Maliasili kutoka Wilaya ya Busega, Bi. Jesca Mathias amesema kuwa kutokana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu Mkoani Simiyu, Serikali inalipa kifuta jasho/machozi kwa waathirika.
 
Amewataka wananchi hao kuhakikisha wanatoa taarifa za majeruhi, vifo au uharibifu wa aina yoyote unaotokana na wanyamapori wakali na waharibifu ili taratibu za malipo zifanyike kwa wakati.
 
"Unapotoa taarifa mapema kwa kiongozi wa kijiji zitajazwa fomu maalum za malipo ambazo zitapelekwa Wizara ya Maliasili na Utalii " amesema Bi.Grace.
 
Kwa upande wake Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii,  Bw. Nassoro Wawa amesema Serikali imeanzisha mfumo wa kielektroniki wa kukusanya taarifa za wananchi wanaopata athari kutokana na changamoto za wanyamapori wakali na waharibifu.
 
Elimu ya uhifadhi na namna ya kukabiliana na changamoto za wanyamapori wakali na waharibifu inaendelea kutolewa Mkoani Simiyu lengo ikiwa ni kuongeza uelewa kwa wananchi kuepuka madhara yatokanayo na wanyamapori hao.
Posted by MROKI On Tuesday, October 07, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo