Nafasi Ya Matangazo

September 28, 2025

Na Mwansldishi Wetu, Geita
Tume ya Madini imeibuka kinara kwa kunyakua tuzo mbili katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili mkoani Geita.

Tuzo hizo ni pamoja na tuzo ya Mdhamini wa Maonesho ya Madini na tuzo ya Mshindi wa Kwanza katika kundi la Taasisi Wezeshi za Serikali katika Sekta ya Madini.

Tuzo hizo zimekabidhiwa na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said, ikiwa ni heshima kubwa kwa mchango wa Tume katika kuimarisha sekta ya madini nchini.

Kupitia tuzo hizo, Tume ya Madini imethibitisha nafasi yake muhimu katika kuwezesha mazingira rafiki ya uwekezaji, usimamizi wa rasilimali, na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa.




Posted by MROKI On Sunday, September 28, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo