Nafasi Ya Matangazo

September 09, 2025







Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Wanariadha Justa Tibendelana wa Mahakama na Paul Remi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) wamekuwa mabingwa wa mbio za mita 3000 kwa wanawake na wanaume katika michuano ya 39 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara,  Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) iliyofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kwa upande wa wanawake Justa aliibuka kidedea kwa kuwashinda Mary Paul wa Wizara ya Katiba na Sheria na wa tatu ni Zamoyoni Komba wa Tume ya Sheria, wakati kwa wanaume Remu aliwashinda Joseph Kachalla wa Wizara ya Afya; na Evarist Gimanya wa RAS Mwanza.
 
Katika mbio za mita 800 kwa wanawake Eudes Kamlali wa Ofisi ya Bunge ameshinda kwa kuwashinda Mgole Amos wa RAS Pwani na Zawadi Mkonga wa Wizara ya Uchukuzi; wakati kwa wanaume Marile Witimu wa TAKUKURU katwaa ubingwa mbele ya Peter Masinde wa RAS Lindi na Hashim Kizigo wa Wizara ya Katiba na Sheria.

Katika mbio za watu wazima wenye umri kuanzia miaka 50 upande wa wanaume Florence Prudence wa RAS Kagera aliibuka wa kwanza akifuatiwa na Ramadhani Sandali wa Mahakama na watatu ni Sailos Lekutu wa Ukaguzi; na wanawake ni Aveline Stephano wa Hazina; huku mshindi wa pili ni Monica Katema wa Bunge na watatu ni Deborah Eliua wa Tume ya Ualimu (TSC).

Kwa upande wa mchezo wa kurusha tufe kwa wanaume Sifael Msenga wa Wizara ya Ujenzi katwaa ubingwa kwa kurusha umbali wa mita 10:37; akifuatiwa na Walter Kapinga wa Ofisi ya Rais Ikulu aliyerusha mita 09:70 na watatu Alfred Mushy wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mita 08:90; wakati wanawake kashinda Enid Geofrey wa TSC kwa umbali wa 7:72, akifuatiwa na Theodatha Salama wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa 7:45 na watatu ni Domina Dominick wa RAS Singida kwa 6:60.

Wakati huo huo, timu zilizofuzu kwa hatua ya robo fainali kwa mchezo wa kuvuta kamba kwa wanawake ni Mahakama wamewavuta Wakili Mkuu (2-0); Wizara ya Uchukuzi waliwashinda Wizara ya Mambo ya Ndani (2-0); TAMISEMI waliwashinda Bunge (1-0); Ofisi ya Mashtaka waliwaliza ndugu zao Tume ya Sheria (2-0), TAKUKURU waliwavuta Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (2-0); RAS Geita wametoa upinzani kwa Wizara ya Madini (2-0); RAS Tanga wamewavuta Wizara ya Afya (2-0) na Tume ya Sheria wamewashinda Ofisi ya Waziri Mkuu Sera (1-0).

Kwa upande wa wanaume timu ya Ofisi ya Rais Ikulu wamewashinda Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (2-0), Mahakama waliwavuta Mashtaka (2-0); Wizara ya Mifugo na Uvuvi waliivuta Wizara ya Elimu (2-0); Waziri Mkuu Sera waliwashinda RAS Iringa (2-0); Hazina waliwaliza Wizara ya Ardhi (2-0); Wizara ya Maji waliibuka kidedea mbele ya Tume Sheria (2-0), TAKUKURU waliwavuta Wizara ya Maliasili na Utalii (2-0) na Wizara ya Uchukuzi waliwashinda Wizara ya Mambo ya Ndani (1-0). 

Katika mchezo wa mpira wa miguu mabingwa watetezi Utumishi SC wamemfunga Wizara ya Mambo ya Ndani kwa bao 1-0;  huku Wizara ya Mambo ya Nje waliwashinda RAS Mara kwa 2-1; nao Wizara ya Ujenzi wameshinda Hazina magoli 6-5 baada kumaliza muda kawaida kwa magoli 2-2 na kupigiana penati; wakati Tume ya Umwagiliaji waliwashinda Wizara ya Maji kwa 4-2; na Ofisi ya Maadili waliwachapa Wizara ya Madini 3-1; Wizara ya Uchukuzi waliwafunga Wizara ya Ardhi kwa 2-0; na TAKUKURU kaibuka mshindi dhidi ya RAS Geita kwa magoli 5-0; nao Katiba na Sheria wamewashinda Wizara ya Afya kwa 5-3.

Katika mchezo wa netiboli mabingwa watetezi Ikulu waliwafundisha Wizara ya Maji kwa 61-1; huku TAMISEMI wakiwafunga wenyeji RAS Mwanza kwa 25-24; nayo Wizara ya Ujenzi waliwafunga Wizara  ya Ardhi kwa 24-20; Wizara ya Mawasiliano wamwafunga  Maendeleo ya Jamii kwa 32-26; Wizara ya Nishati kafungwa na Mahakama kwa 34-27; Ukaguzi wamewashinda kwa mbinde Hazina kwa 27-26.
Posted by MROKI On Tuesday, September 09, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo