Nafasi Ya Matangazo

August 30, 2025

Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi amewasili mkoani Mara,akianza kwa kuwasalimia Wananchi wa Bunda mjini leo Jumamosi Agosti 30,2025  mkoani humo kuendelea na kampeni zake  mara baada ya kumaliza mkoa wa Mwanza.

Baada ya kuwasalimia Wananchi wa Bunda mjini,Balozi Dkt.Nchimbi akiwa ni mgombea mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pia aliwanadi Wagombea wa Mkoa huo akiwemo  mgombea Ubunge wa Jimbo la Bunda mjini, Easter Bulaya  pamoja na Wagombea wa Udiwani .

Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi yupo kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya Kufanya Kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.











Posted by MROKI On Saturday, August 30, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo