Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ameshiriki
na kuhutubia Kongamano la PPRA lililolenga kujadili Ununuzi wa umma na Ukuzaji wa
kampuni za wazawa na makundi maalum kwa ukuaji wa Uchumi Jumuishi katika zama
hizi za mabadiliko ya teknolojia/ Kidigitali
Kongamano hilo
limefanyika Juni 16, 2025 Jijini Arusha ambapo katika hotuba yake Kikwete
amesisitiza umuhimu
wa kuendelea kutambua mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa na Serikali ya Awamu
ya Sita inayoongozwa na Dr. Samia Suluhu Hassan , Rais Wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ambayo pamoja na mambo mengine yanalengwa kuwasaidia
na kukuza ustawi wa Watu wenye mahitaji maalum.
Kikwete alibainisha kwa kuwakumbusha
mambo 6 yaliyofanywa na Serikali ya awamu
ya sita katika kuwawezesha vijana na watu wenye ulemavu ili
waweze kujiinua kiuchumi ikiwemo maelekezo ya kisheria ya kuendelea kutenga asilimia
30 ya zabuni za ununuzi wa umma.
Aidha, aliwakumbusha umuhimu wa kutoa
elimu na kuwashirikisha wadau muhimu katika jamii wakiwemo Madiwani na
Wakurugenzi wa Halmashauri, Manispaa na Majiji ili elimu ya kuwepo kwa fedha
maalum zinazotengwa toka kwenye manunuzi ya Umma ijulikane.
“Moja ya changamoto
kubwa kwa sasa ni ufahamu hafifu wa kuwepo kwa fedha hizi. Umuhimu na msisitizo
kama huu umesaidia sana vijana, wanawake na wenye ulemavu kukimbilia zile
asilimia 10 zinazotengwa na Halmashauri kutoka kwenye mapato ya ndani,”alisema Kikwete.
0 comments:
Post a Comment