Nafasi Ya Matangazo

April 05, 2025

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza nafasi za kazi za mratibu wa uchaguzi, msimamizi wa uchaguzi na msimamizi msaidizi wa uchuguzi ngazi ya jimbo watakaosimamia Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara kwa upande wa Tanzania Zanzibar
Kwa mujibu wa tangazo la Tume lililosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima, R. K, nafasi hizo ni kwa Unguja na Pemba na wanaotakiwa kuomba nafasi hizo ni raia wa Tanzania, watumishi wa umma na sifa nyingine zilizoainishwa kulingana na nafasi inayoombwa.
Tangazo hilo limemtaka kila mwaombaji aainishe nafasi anayoiomba, akitaja wilaya au jimbo analotaka kufanyia kazi na aambatishe vyeti vya elimu pamoja na maelezo binafsi (CV) na maombi yatapokelewa kuanzia tarehe 3 Aprili, 2025 hadi tarehe 23 Aprili, 2025 saa 9:30 Alasiri.
Maombi hayo yanatakiwa kuwasilishwa katika Ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Maisara kwa upande wa Unguja na Chakechake (Mtaa wa Miembeni) kwa upande wa Pemba kwa anuani ya Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ofisi ya Zanzibar, Mtaa wa Maisara, S. L. P 4670, Zanzibar. SOMA ZAIDI.   

Posted by MROKI On Saturday, April 05, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo