Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Philip Mpango aliuwasha mwenye wa Uburu Aprili 2,2025 katika viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, Mkoani Pwani.
Mapema wakati wa sherehe hizo za kuwasha Mwenge kwa mwaka huu wa 2025 kulitanguliwa na hotuba na salaam mbalimbali kutoka kwa viongozi.
Waziri Mwenye dhamana ya mwenge huo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete alipata fursa ya kuzungumza ambapo pamoja na mambo mengine aliwaeleza kuhusu alama ya uzalendo kwa Watanzania kutoka katika mwenge wa Uhuru.
Alizungumza hayo mbele ya Wananchi waliojitokeza na Viongozi wa Kitaifa wakiongozwa na Aliyekuwa Mgeni Rasmi wa Shughuli hiyo Dr. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyefuatana na Viongozi mbalimbali akiwemo Ndg. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu, Dr. Dotto Biteko , Naibu Waziri Mkuu na Waziri Wa Nishati na Alhaj Hamza Juma , Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Pili, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliiwakimbusha Watanzania Umuhimu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ambao unatokana na Ujumbe unaosambaza.
Pia kuwakumbusha Ujumbe wa Mwenge Mwaka huu ambao ni "Jitokeze Kupiga Kura Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu" huku zile jumbe nyengine ikiwemo ya mapambano dhidi ya Rushwa, maradhi kama VVU/Ukimwi, Malaria, Lishe zikiwa bado zinaendelea.
Dr. Philip Isdor Mpango, mgeni rasmi alitumia nafasi hiyo kuwahimiza viongozi na wanaosimamia shughuli za uchaguzi kuhakikisha haki inatolewa na kuondoa hali za kuchafua amani.
Mwenge wa Uhuru uliwashwa na kuukabidhiwa kwa viongozi wa Mkoa wa Pwani ambapo Mkuu wa Mkoa Alhaj Aboubakar Kunenge alikulat kiapo cha kuukimbiza mwenge kwenye halmashauri 9 za Mkoa wa Pwani.
Mbio hizi za Mwenge wa Uhuru zilizowashwa Kibaha, Pwani zinatarajiwa kuhitimishwa Mkoani Mbeya tarehe 14 Oktoba 2025 baada ya kutembea, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri 195, katika Mikoa 31 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment