Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Vyama vya Wafanyakazi ni nguzo muhimu katika kujenga mahusiano yenye tija mahali pa kazi.
Amebainisha hayo leo Machi 3, 2025 Jijini Dodoma katika mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli na Shughuli zinazohusiana na Reli (RAWUTA), ambapo amesema kuwa Vyama hivyo vya Wafanyakazi ni vyombo vinavyotetea masuala yote yanayogusa maslahi na haki zao za msingi. “Vyama vya Wafanyakazi nchini vimeendelea kuimarika na kuwa nguzo muhimu katika kusimamia maslahi ya Watumishi na Utatuzi wa migogoro, hivyo mazingira ya kazi yanakuwa bora kwa ustawi wa wafanyakazi na maendeleo ya taifa kwa ujumla,” amesema.
Aidha, Mhe. Kikwete amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira ya kukuza ustawi wa vyama vya Wafanyakazi mahali pa kazi sambamba na kuendelea kuhamasisha uanzishwaji wa mabaraza ya Wafanyakazi ili kuweka mfumo mzuri wa majadiliano baina ya waajiri na Waajiriwa.
Vile Vile, Waziri Kikwete amesema serikali itaendelea kushirikiana na wadau kutoa elimu ya masuala ya kazi ili kupunguza migogoro katika eneo la kazi na kujenga uelewa wa haki na wajibu wa Waajiri na Waajiriwa.
Kwa upande mwengine, amekipongeza chama cha pongeza wa Chama cha (RAWUTA) kwa kushirikiana na katika mipango na mikakati ya kukuza miradi inayohusu miundombinu ya reli kwa ajili ya kuwezesha huduma ya usafiri na usafirishaji nchini.
0 comments:
Post a Comment