Shirika la Reli Tanzania (TRC) linautaarifu Umma juu ya kukamilika kwa majaribio ya mabehewa 264 ya mizigo, yaliyowasili nchini Desemba 2024.
Majaribio ya mabehewa hayo yaliyochukua mwezi mmoja yaliyofanyika kwa kujumuisha mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini (LATRA), yalijikita katika maeneo mawili ambayo ni tuli (static) na mwendo (dyanamic).
Lengo la majaribio hayo ilikuwa ni kuangalia umadhubuti likiwa linatembea.
Wakati wa zoezi hilo LATRA imefanya kaguzi za mabehewa yote 264 kati ya hayo 200 yakiwa ni ya makasha (containers carriers) na 64 ni ya mizigo isiyofungwa (loose cargoes).
Aidha LATRA imejiridhisha kuwa ubunifu wa mwendokasi (design speed) wa kilometa 120 kwa saa umefikiwa na kuthibitisha kuwa yamefanya vizuri katika mifumo yote muhimu ikiwemo breki na kwenye kona (curve).
Katika hatua nyingine LATRA imesema itatoa ithibati kwa TRC, kama sheria na kanuni zinavyotamka ili mabehewa haya yaanze kubeba na kusafirisha mizigo.
Kukamilika kwa majaribio ya mabehewa hayo 264 kati ya 1,430 yanayotengenezwa na kampuni ya CRRC ya China, ni kiashiria kuwa usafirishaji mizigo katika reli ya kiwango cha kimataifa ( SGR) uko mbioni kuanza.
0 comments:
Post a Comment