WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 4,2025 jijini Dodoma kuhusu Sensa ya uzalishaji viwandani kwa mwaka wa rejea 2023.
Na.Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt. Selemani Jafo,amesema Tanzania inatarajia kufanya sensa ya uzalishaji wa viwandani kuanzia machi mwaka huu.
Dkt.Jafo ameyasema hayo leo Februari 4,2025 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sensa hiyo ya uzalishaji viwandani kwa mwaka wa rejea 2023.
Amesema lengo la sensa hiyo ni kupata taarifa za kina za kitakwimu zitakazo iwezesha serikali na wadau kufanya maamuzi yenye ushahidi wa kitakwimu katika kuhuisha na kuboresha sera, mipango na program za maendeleo ya sekta ya viwanda na uchumi wa kitaifa kwa ujumla.
“Matokeo hayo yatatumika kupima utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano (FYDP III), program za kikanda kama vile Dira ya Afrika Mashariki 2050, Agenda ya Maendeleo ya Afrika 2063.
“Na Malengo endelevu ya Dunia 2030 (SDGs) hususani lengo namba sita kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama, lengo namba saba kuhusu upatikanaji wa nishati safi na ya gharama nafuu na lengo namba tisa kuhusu maendeleo ya viwanda, ubunifu na miundombinu,”amesema Dkt. Jafo
Hata hivyo amesema kuwa Sensa hiyo itakusanya taarifa kutoka viwanda vyenye wafanyakazi kuanzia 10 au zaidi na kundi la viwanda vyenye wafanyakazi kuanzia mmoja hadi tisa.
Amesema kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi kwa viwanda vidogo zitafanyika kwa sampuli kutokana na wingi wa viwanda na sifa zinazofanana.
“Ukusanyaji wa taarifa za uzalishaji wa bidhaa viwandani utafanyika kwa kutumia mfumo wa kielektroniki ambapo wadadisi watakusanya taarifa kwa kutumia madodoso yaliyowekwa kwenye kishikwambi kama ilivyofanyika wakati wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022’”amefafanua
Aidha ametoa wito kwa wadau wote katika sekta ya viwanda nchini kushirikiana na serikali kufanikisha utekelezaji wa sensa hiyo ya uzalishaji viwandani.
Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk. Albina Chuwa, amesema sensa hiyo inatarajiwa kufanyika kwa muda wa miezi mitatu kuanzia mwezi Machi hadi Juni mwaka huu ambapo majibu yatatolewa.
"Sensa hiyo ambayo imepangwa kufanyika kuanzia mwezi Machi mwaka huu, itahusisha pande zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."amesema Dk. Chuwa
Tanzania Bara, ilifanya sensa za uzalishaji viwandani mwaka 1963, 1978, 1989 na 2013 na kwa upande wa Zanzibar zilifanyika mwaka 1989, 2002, 2008 na 2012.
WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 4,2025 jijini Dodoma kuhusu Sensa ya uzalishaji viwandani kwa mwaka wa rejea 2023.
WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 4,2025 jijini Dodoma kuhusu sensa ya uzalishaji viwandani kwa mwaka wa rejea 2023.
WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt. Selemani Jafo,akisisitiza jambo wakati akielezea sensa ya uzalishaji viwandani kwa mwaka wa rejea 2023 leo Februari 4,2025 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt. Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati akizungumza kuhusu Sensa ya uzalishaji viwandani kwa mwaka wa rejea 2023 leo Februari 4,2025 jijini Dodoma.

Mtawimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na Waandishi wa habari wakati wa Mkutano wa Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt. Selemani Jafo,akitangaza kuanza kwa Sensa ya uzalishaji viwandani kwa mwaka wa rejea 2023 leo Februari 4,2025 jijini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment