Nafasi Ya Matangazo

December 12, 2024

MENEJA EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi. Walter Christopher, amewahamasisha wamiliki wa vituo vya mafuta kupeleka huduma ya nishati safi ya kupikia vijijini ili kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mhandisi Christopher ametoa wito huo wakati wa mafunzo ya siku moja kwa wadau wa mafuta Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga .

Mhandisi Christopher amesema kuwa Serikali inaendelea kuhamasisha wananchi kutumia Nishati Safi ya kupikia ili kulinda afya, kuokoa gharama na muda sambamba na kulinda Mazingira.

"Nishati Safi ya kupikia ina manufaa makubwa kwetu binadamu na mazingira kwa ujumla hivyo nawaomba wamiliki wa vituo vya mafuta muunge mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kupeleka huduma hiyo kwa wananchi wa vijijini ili waweze kutumia nishati safi ya kupikia."amesema Mhandisi Christopher

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAPSOA Wilaya ya Kahama, Bw. Alley Abeid Salum ameishukuru EWURA kwa elimu na anaamini kuwa itatoa majibu ya changamoto zinazowakabili wadau wa mafuta.

Posted by MROKI On Thursday, December 12, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo