Nafasi Ya Matangazo

October 03, 2024





Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Wachezaji Musa Chilendi wa Wizara ya Uchukuzi na Niuka Chande wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wametwaa ubingwa wa mchezo wa draft kwa wanawake na wanaume katika michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) inayofanyika mkoani Morogoro.

Musa mchezaji chipukizi amemfunga mkongwe Gervas Mwashimaa wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika mchezo mkali wa fainali kwa pointi 2-1. 

Ushindi wa tatu kwa wanaume umechukuliwa na Ishengoma Kiliba wa Wizara ya Mambo ya Ndani aliyemfunga Ishara Charles wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa pointi 1-0.

Kwa upande wa wanawake Niuka wa Mawasiliano amemfunga mpinzani wake  Pulkeria Maimu wa TAMISEMI  kwa pointi 2-1. Wachezaji hawa walikutana fainali katika michezo ya mwaka 2023 na Niuka akaibuka bingwa.

Ushindi wa tatu kwa wanawake umechukuliwa na Badaka Kabaka wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliyemfunga Mizowa Wemena wa Wizara ya Ujenzi.
Posted by MROKI On Thursday, October 03, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo