NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amepongeza Tume ya Madini kwa kuendelea kuvuka lengo la ukusanyaji wa maduhuli na kusisitiza kuendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha wanavuka lengo walilopewa na Serikali la kukusanya kiasi cha shilingi Trilioni Moja katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Oktoba 05, 2024 alipotembelea banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake akiwa ameambatana na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde katika Maonesho ya Saba ya Kitaifa ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini Geita yaliyoanza Oktoba 2, kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita.
"Mnafanya kazi nzuri sana Tume ya Madini, lengo mlilopewa ni kukusanya Shilingi Trilioni Moja katika mwaka wa fedha 2024/2025, naamini mtalivuka," amesema Dkt. Biteko.
Taasisi nyingine chini ya Wizara ya Madini zinazoshiriki katika maonesho ni pamoja na Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia ( TEITI), Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania ( GST) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)
0 comments:
Post a Comment